KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, September 13, 2011

Zlatan Ibrahimovic OUT DHIDI YA BARCELONA.

Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic hatojumuishwa kikosini usiku huu katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo AC Milan watakua ugenini wakipambana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo FC Barcelona.

Zlatan Ibrahimovic hatokuwepo kikosini baada ya kuthibitika hatoweza kucheza mchezo wa usiku huu kufautia maumivu ya nyonga yanayomkabili toka mwishoni mwa juma lililopita.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Ac Milan zimeeleza kwamba jopo la madaktari wa klabu hiyo lilikua na kazi ya ziada kuhakikisha mshambuliaji huyo anacheza mpambano dhidi ya Fc Barcelona lakini hatua hiyo imeshindikana.

Hata hivyo bado haijafahamika kama atakuwepo katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo AC Milan wataendelea kuutetea uibingwa wao wa nchini Italia kwa kuwakaribisha SS Napoli huko San Siro.

Kuumia kwa Zlatan Ibrahimovic, kunaacha maswali mengi kwa mashabiki wa AC Milan ambao sasa wanawatazama washambuliaji wawili pekee ambao ni Alexandre Pato pamoja na Antonio Cassano ambapo hatua hii inakuaja kufuatia kuenguliwa kwa mshambuliaji mkongwe Filippo Inzaghi ambae jina lake halikusajili kwa ajili ya michuano ya barani ulaya.

Nae mshambuliaji kutoka nchini Brazil Robinson Robinho hatokuwepo katika mpambano wa hii leo kutokana na kuwa majeruhi.

Katika hatua nyingine menaja wa AC Milam Massimiliano Allegri amesema usiku huu wanakwenda kupambana na kikosi bora ambacho kinastahili sifa za ushindi lakini akaahidi kuwahiza wachezaji wake kucheza kwa kujituma na kusaka ushindi ugenini.

Amesema hakuna duniani asifahamu kuhusu Fc Barcelona, lakini anaamini ubora wa kikosi chake pia utaweza kuleta upinzani mkubwa na kusababisha mchezo mzuri wakati wote wa dakika 90.

No comments:

Post a Comment