KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, October 3, 2011

BAKARI NJE MIEZI MITATU !!!

Beki wa pembeni wa klabu ya Arsenal Bacary Sagna, itamchukua muda wa miezi miwili hadi mitatu kurejea tena uwanjani baada ya kuumia akiwa katika mchezo wa jana wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Tottenham Hotspurs walioibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja.

Daktari wa timu ya taifa ya Ufaransa Fabrice Bryand amethibitisha taarifa hizo kwa kusema kwamba Bacary Sagna hatokuwepo katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili, ambapo mabingwa hao wa dunia wa mwaka 1998, watacheza mchezo wa kuwania nafasi kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi ya Albania.

Daktari huyo ametoa taarifa hizo kwa kushirikiana na jopo la madaktari wa klabu ya Arsenal ambao pia wamethibitisha kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 28 amevunjia mfupa wa mguu uitwao Fibula.

Tayari kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Blanc ameshamuita kikosini beki wa pembeni wa klabu Lille Mathieu Debuchy kama mbadala wa Bakari Sagna kwa ajili ya kuendelea na kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya.

Bakari Sagna aliumia mguu baada ya kusukumwa na beki wa pembeni wa Tottenham hotspurs Benoit Assou-Ekotto hatua ambayo ilimfanya kuangukia mbao za matangazo pembezoni mwa sehemu ya kuchezea ya uwanja wa White Hart Lane.

Wakati huo huo viongozi wa klabu ya Arsenal pamoja na Spurs wamelaani vitendo vya ubaguzi wa rangi vilivyojitokeza katika mchezo wa jana pale klabu hizo zilipokutana huko kaskazini mwa jiji la London.

Viongozi wa pande hizo mbili wamesema daima wataendelea kushirikiana kwa kila hali na katu hawatochukizana eti kwa sababu ya mashabiki ambao walionyesha vitendo ambavyo vilikosa uungwana.

Kwa mujibu wa taariffa iliyotolewa kwa pamoja na pande hizo mbili inadai kwamba lugha za matusi, kejili pamoja na ubaguzi wa rangi zilitawala kwa mashabiki wa Arsenal pamoja na wale wa Spurs.

Kwa upande wa Arsenal walimkejeli mshambuliaji wao wa zamani Emmanuel Adebayor kwa kumzomea na kumuimbia nyimbo za kumkashifu kutokana na janga lililoikuta timu ya taifa ya Togo ilipokua ikielekea nchini Angola katika fainali za mataifa ya barani Afrika mwaka 2010.

Nao mashabiki wa Spurs waliwakashifu wachezaji wa Arsenal Alex Song pamoja na Bakari Sagna kwa kigezo cha rangi.

3 comments:

  1. ดูหนัง Angel Has Fallen ผ่ายุทธการ ดับแผนอหังการ์ (2019) ได้ที่นี่ แสนสนุกได้ทุกที่ ดูหนังฟรีไม่มีจำกัด
    https://www.doonung1234.com/

    ReplyDelete
  2. เล่นเกมยิงปลาออนไลน์แสนสนุกที่นี่สิ

    https://www.slotxd.com/%e0%b9%80%e0%b8%81%e0%b8%a1%e0%b8%a2%e0%b8%b4%e0%b8%87%e0%b8%9b%e0%b8%a5%e0%b8%b2

    ReplyDelete