KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, October 4, 2011

BONGE LA BIFU NDANI YA FULHAM.

Meneja wa klabu ya Fulham Martin Jol ameingia katika vita kali na baadhi ya wachezaji wake baada ya kuwatoza faini ya paund 500, kufuatia kitendo cha kukosa penati katika mchezo wa mzunguuko wa tatu wa kombe la ligi *Curling Cup* dhidi ya Chelsea mnamo September 21.

Martin Jol ameamua kufanya hivyo akichulia kama sehemu ya kuwafunda wachezaji wake ili waweze kutambua umuhimu wa kusaka ushindi pale inapohitajika na si kufanya vitendo vya kizembe na kuigharimu klabu inayowategemea kwa kiasi kikubwa.


Mmoja wa maafisa wa klabu ya Fulham amesema kitendo hicho kimewakera mno wachezaji waliokatwa pesa hizo, hatua ambayo inaendeleza upinzani miongoni mwao dhidi ya Martin Jol alietangazwa kuchukua nafasi ya Mark Hughes miezi miwili iliyopita.

Orlando Sa mshambuliaji kutoka nchini Ureno alikosa mkwaju wa penati katika muda wa kawaida baada ya kuangushwa katika eneo la hatari, hatua ambayo iliinyima nafasi Fulham kusonga mbele kupitia muda wa kawaida.

Nae Pajtim Kasami kiungo kutoka nchini Macedonia alikosa mkwaju muhimu wa penati baada ya timu hizo kwenda sare ya bila kufungana katika muda wa dakika 120, hatua ambayo ilitoa mwanya kwa Chelsea kuendelea katika michuano ya kombe la ligi.

Itakumbukwa kwamba penati ya Kasami iligonga mwamba na kuifanya Chelsea kupata ushindi wa peneati 4-3.

2 comments: