
Tottenham Hotspur wamekubalia dili la kumsajili beki wa klabu ya Newcastle United Sebastien Bassong kwa ada ya uhamisho wa paund million 8.
Taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu ya Tottenham Hotspur zimeonyesha kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kukamil;isha uhamisho wake, endapo atapita katika vipimo vya afya yake.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kurejea katika timbwili timbwili la ligi kuu msimu ujao baada ya klabu yake ya sasa kushuka daraja msimu uliopita.
Beki huyo wa kimataifa toka nchini Cameroon, ambae pia anweza kucheza nafasi ya beki wa kushoto, anatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya Spurs ambayo ina wachezaji kama Jonathan Woodgate, Michael Dawson pamoja na Ledley King ambae hata hivyo yu mashakani kucheza michezo ya awali ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambayo yataraji kuanza kutimu vumbi lake August 15.
No comments:
Post a Comment