Kuondoka kwa kiungo huyo ni pigo kubwa kwa viongozi wa wekundu hao licha ya kuwa pengine uongozi huo unaandaa mikakati ya kuziba pengo lililoachwa na Alonso.
Aidha klabu hiyo pia inataraji kurudisha fedha zilizolipwa baada ya kuuza picha cha Alonso wakati akitambulisha jezi mpya za klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Madrid nchini Hispania Xavi Alonso amesema anawaheshima na ataendelea kuwaheshimu mashabiki wa klabu ya Liverpool kwa ushirikiano waliomuonyesha kwa miaka mitano aliyoichezea klabu hiyo na hana cha kuwalipa zaidi ya shukurani.
Akijibu kuhusu uhusiano wake na meneja Rafa Benitez ambao unadaiwa kuwa ndio sababu ya kuihama klabu hiyo , Alonso amesema yapo mambo mengi yaliyozungumzwa katika vyombo vya habari lakini ukweli ni kwamba wakati ulifika wa kubalisha maisha na kutafuta klabu nyingine katika kuendelea kipaji chake cha kucheza soka. 
Wakati huo huo XABI ALONSO amebotoa siri kwa kueleza yale yaliyompelekea kuondoka Anfiled yalipo makao makuu ya klabu ya Liverpool na kuelekea St Bernabeu yalipo makao makuu ya Real Madrid.
Alonso pamoja na kuwa mawazo ya kuelekea Real Madrid kwa kipindi kirefu kilichopita alifanya mazungumzo Rafael Benitez na kumueleza angependa kuhama ili aweze kukabiliana na changamoto nyingine katika maisha yake ya soka.

Alonso pia amebainisha sababu nyingine ya kuondoka anfield imetokana na Benitez kutaka kumuuza katika klabu ya Juventus msimu uliopita ili aweze kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Man City Gareth Barry ambapo msimu uliopita alikuwa akiichezea klabu ya aston Villa.
Kuhusu kuhamia katika klabu ya Real Madrid Alonso amesema ni hatua kubwa katika maisha yake ya soka ambapo ametoka kwenye klabu kubwa na kuijunga na klabu nyingine kubwa.
Alonso mwenye umri wa miaka 27 amesaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Real Madrid baada ya kukamilisha uhamisho wenye gharama ya paundi milioni 30 na atakuwa analipwa kiasi cha paundi elfu 85, kwa juma.

Hata hivyo imeelezwa kuwa mara baada ya kufanyiwa vipimo kiungo huyo alijiunga na wachezaji wenzake kufanya mazoezi ambao walisimama kwa heshima mara baada ya kuwasili katika kambi hiyo.
No comments:
Post a Comment