Monday, June 7, 2010

BENITEZ KUJIUNGA NA INTER MILAN?


Aliekua meneja wa klabu ya Liverpool Rafael Benitez yu mbioni kuanza mazungumzo na viongozi wa klabu bingwa barani Ulaya Inter Milan.

Benitez anaelezwa huenda akafikia makuabaliano na viongozi wa klabu hiyo kati kati ya juma lijalo.

Akizungumza juu ya utaratibu wa meneja huyo, raisi wa klabu ya Inter Milan Masimo Morati amesema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha utaratibu wa kuanza mazungumzo hivyo anaamini yatakwenda sawia kama walivyopanga.

Itakumbukwa kuwa Benitez kibarua chake ndani ya klabu ya Liverpool kilifikia kikomo kati kati ya juma hili baada ya kupungiwa mkono wa kwa heri na viongozi wa klabu hiyo ya nchini uingereza.

No comments:

Post a Comment