Beki wa kimataifa toka nchini Brazil na klabu ya Inter Milan Maicon amesisitiza kuendelea kubaki kwenye klabu yake msimu ujao kama mkataba wake unavyoeleza.
Maicon ametoa msisitizo huo kufuatia taarifa zinazomuandama juu kutaka kujiunga na klabu ya Real Madrid iliyo chini ya meneja wake wa zamani Jose Mourinho.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema taarifa za yeye kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Real Madrid ni uzushi mtupu na wala hatothubutu kufuata nyayo za meneja wake Jose Mourinho.
Mbali na kutoa msisitizo huo, Mbazil huyo amevitaka vyombo vya habari kuacha kulizungumzia suala la yeye kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Real Madrid na endapo zitaendelea kutangazwa anajihisi kutokutendewa haki.
Mkataba wa Maicon na klabu ya Inter Milan bado unaendelea kudumu hadi mwaka 2014, ambapo amesema bado ni mwenye furaha kuendelea kuishi katika jiji la Milan huko nchini Italia.

No comments:
Post a Comment