Saturday, June 5, 2010

OBI OUT.

Kiungo wa klabu ya Chelsea John Obi Mikel amejiondoa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria ambacho kipo kambini kikijiandaa na fainali za kombe la dunia za mwaka 2010.

Akitoa sababu zilizoelezwa na kiungo huyo kabla hajaruhusiwa kuondoka kwenye kikosi cha Super Eagles, msemaji wa timu ya taifa ya Nigeria amesema Mikel amehofia maisha yake ya soka kufuatia jeraha la goti lililokua likimsumbua kwa muda mwezi mmoja uliopita.

Hata hivyo msemaji huyo amesema Obi Mikel alikua anashiriki mazozi na wenzake kama kawaida lakini kwa hatua aliyofikia imewasikitisha na hakuna namna ya kuikwepa.

Kuondoka kwa Mikel Obi katika kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria sasa kunatoa nafasi kwa mshambuliaji wa klabu ya (SOSHO) Sochaux ya nchini Ufaransa Brown Ideye.

Kwa maamuzi hayo ya Mikel mwenye umri wa miaka 23, yanamfanya ajiunge na wachezaji wenzake wa klabu ya Chelsea toka barani Afrika Michael Essien, Didier Drogba pamoja na mmoja toka barani Ulaya Michael Ballack watakaozikosa fainali za mwaka huu.

No comments:

Post a Comment