KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 11, 2009

CHAMAKH HUENDA AKAJIUNGA NA ARSENAL.


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameongeza ofa ya paund million 8 ili aweze kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Morroco na klabu ya Bordeaux Marouane Chamakh.

Wenger ameongeza ofa hiyo, baada ya ofa yake ya kwanza ya paund million 6 kukataliwa na uongozi wa klabu ya Bordeaux.

Kufuatia kuongezwa kwa ofa hiyo, taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Bordeaux umeonyesha nia ya kuwa tayari kuketi chini na uongozi wa klabu ya Arsenal kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kumuuza Chamakh mwenye umri wa miaka 25.

Katika hatua nyingine beki wa kimataifa toka nchini Ivory Coast pamoja na klabu ya Arsenal, Emmanuel Eboue amekubali kusalia Emirates baada ya kufanya mazungumzo na meneja wake Arsene wenger.


No comments:

Post a Comment