KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, October 1, 2011

URENO KUWAKOSA WACHEZAJI MUHIMU KIKOSINI.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ureno, kitaelekea katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya, dhidi ya timu ya taifa ya Iceland mwishoni mwa juma lijalo huku kikiwakosa wachezaji wawili wa klabu ya Real Madrid.

Kikosi cha Ureno kitawakosa Pepe pamoja na Fabio Coentrao ambao kwa sasa wanauguza majeraha ya misuli waliyoyapata wakiwa na klabu ya Real Madrid.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ureno Paulo Bento amethibitisha taarifa hizo kwa kusema ameumizwa sana na hatua hiyo lakini hana budi kukubaliana na ukweli uliopo na kutazama ni vipi atakavyoweza kuwakabili Iceland siku ya ijumaa.

Amesema anadhani kwa sasa ni wakati wa kumtumia beki wa FC Köln ya nchini Ujerumani Henrique Sereno, pamoja na beki wa Valencia Ricardo Costa ambao ana hakika wana uzoefu wa kutosha wa kucheza michuano ya kimataifa.

Maamuzi ya meneja huyo pia yameendelea kuheshimu adhabu aliyopewa beki Ricardo Carvalho ambae alisimamishwa na chama cha soka nchini Ureno, kwa muda wa mwaka mzima baada ya kutoroka kambini na kisha kushindwa kutoa sababu zilizopelekea kufanya hivyo.


Katika hatua nyingine Paulo Bento amemuita kikosini winga wa Sporting Clube de Portugal Ricardo Quaresma pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Benfica ambae kwa sasa anaitumikia Sporting Clube de Braga Nuno Gomes.

Timu ya taifa ya ureno ipo katika mazingira mazuri ya kupata nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya baada ya kufikisha point 13, ikiwa sawa na timu ya taifa ya Denmark pamoja na Norway.

No comments:

Post a Comment