KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, July 18, 2009

DAVID BECKHAM AMKANYA JOHN TERRY.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya LA Galaxy DAVID BECKHAM amemuonya beki John Terry afikirie kwa makini kabla ya kufanya uamuzi wa kuihama klabu yake ya Chelsea.

Beckham anatambua maumivu ya kuihama klabu ambayo alikuwa akiishabikia na kuichezea kwa muda wa miaka 10 ya Man utd na kuchukuwa maamuzi ya kujiunga na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 amekumbushia jinsi alivyokuwa na ndoto ya kutaka kuichezea klabu ya Manchester utd maisha yake yote ya soka lakini haikuwa dhamira yake kuondoka Old Trafold bali ilimlazimu kuchukua hatua hiyo.


Amesema kufuatia mapenzi aliyokuwa nayo dhidi ya Man utd ilifikia wakati alikuwa amashindwa kuitazama klabu hiyo kupitia runinga kufuatia hatua ya kuumizwa na kitendo cha kuondoka klabuni hapo.

Beckham amesema mchezo wa soka una maajabu yake na mambo hujitokeza na kuubadilisha kubadilika wakati wowote lakini hadhani kama John Terry ataihama Chelsea kutokana na umuhimu wake ndani ya klabu hiyo.

Becks amesema mamilioni ya klabu ya Manchester City hayataweza kumfanya Terry kuwa na furaha aliyokuwa nayo kwa sasa hivyo amempa ushauri wa kuendelea kuwa na nia ya kuichezea klabu yake yake ya chelsea.


Becks amesema kwa jinsi anavyomfahamu "JT' yaani John Terry alivyo na mapenzi na mchezo wa soka na sio pesa atafanya uamuzi ambao utakuwa na manufaa kwake.


No comments:

Post a Comment