Monday, November 23, 2009

SPURS YAWATOA KAFARA WIGAN.

Tottenham 9 -1 Wigan




Bolton 0- 2 Blackburn

Saturday, November 21, 2009

ENGLISH PREMIER LEAGUE YAREJEA.

Friday, November 20, 2009

BORA TURUDIANE !!!!!!!!


Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry amesema ombi la jamuhuri ya Ireland la kutaka mchezo urudiwe ni la kiungwana na endapo FIFA watabadili maamuzi yao wao wapo tayari.

Henry amesema hatua ya kurudiwa kwa mchezo huo ni nzuri ambayo anaamini aitamaliza malalamiko yaliyojitokeza miongoni mwa mashabiki pamoja na viongozi wa nchi ya Ireland.

ANGOLA KUMEIVA.


Makundi ya michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika ya mwaka 2010 hii leo yamapangwa huko nchini Angola itakapofanyika michuano hiyo mapema mwakani.


Group A: Angola, Mali, Algeria, Malawi.

Group B: Ivory Coast, Ghana, Togo, Burkina Faso.

Group C: Egypt, Nigeria, Benin, Mozambique.

Group D: Cameroon, Tunisia, Zambia, Gabon.



Baada ya kupangwa kwa michuano hiyo ratiba inaonyesha kwamba wenyeji wa fainali hizo timu ya taifa ya Angola itafungua michuano hiyo kwa kucheza na timu ya taifa ya Mali.


MISRI KUADHIBIWA?


Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA imeeanza kuchunguza vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyojitokeza kwenye mchezo wa pili kati ya timu ya taifa ya Misri dhidi ya Algeria uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita mjini Cairo.

Kamati hiyo inachunguza vitendo hivyo kufuatia taarifa za kuumizwa kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Algeria ambao waliripotiwa kupigwa na watu wasiojulikana.

FIFA wamesema kitendo hicho kinachochunguzwa kilitoea mara baada ya wachezaji wa timu ya taifa ya Algeria kuwasili jijini Cairo tayari kwa mchezo huo uliomalizika kwa kushuhudia Misri wakiibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

FIFA YAONYESHA MSIMAMO.


Shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA limeyaweka kapuni maombi ya chama cha soka cha jamuhuri ya Ireland ya kutaka mchezo wa mtoano kati yao na Ufaransa urudiwe.

Ombi hilo la chama cha soka cha jamuhuri ya Ireland limewasilishwa jana baada kuzuka kwa utata wa maamuzi bao lililofungwa na William Gallas, ambae alipokea pasi kutoka kwa Thierry Henry alieunawa mpira mara mbili.

Chanzo cha habari toka ndani ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA kimeeleza kuwa hakuna njia yoyote ambayo itakubaliana na ombi la Jamuhuri ya Ireland hivyo matokeo yaliyopatikana katika mchezo wa jumatano yatasalia kama yalivyo.

Thursday, November 19, 2009

EDUARDO AFUTA NDOTO ZA LIVERPOOL.

Eduardo akisaini mkataba mpya akiwa na mtendaji mkuu wa klabu ya Arsenal Ivan Gazidis.



Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Croatia na klabu ya Arsenal Eduardo amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kusalia Ashburton Grove.

Eduardo amesaini mkataba huo huku akiwa anahusishwa na taarifa za kutakiwa kwa udi na uvumba na klabu ya Liverpool ambayo kwa sasa inakwenda mzobe mzobe kwenye michuano kadha wa kadha barani Ulaya.

Akizungumzia hatua ya kusaini mkataba wa mshambuliaji huyo, meneja wa klabu ya Arsenal Arsene wenger, amesema Eduardo ni mchezaji anaetazama mbali katika maisha yake ya soka na ndio maana amekubali kuendelea kusalia huko Emirates.

HENRY AZUA UTATA.


Beki wa timu ya taifa ya jamuhuri ya Ireland amelalamikia kitendo cha udanganyifu kilichofanywa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry cha kushika mpira mara mbili kabla ya kutoa pasi iliyozaa goli la kusawazisha lililofungwa William Gallas.

Dunne amesema Henry hakufanya kitendo cha uungwana cha kuunawa mpira na kushangilia mara baada ya bao kupatikana.

Beki huyo amesema pamoja na kusaka bao la kusawazisha ambalo lilikua likihitajika sana upande wa wapinzani wao bado Henry ambae anafahamika ulimwenguni kwa uwezo wake wa kucheza soka hakustahili kufanya kitendo hicho ambacho kimeonekana na wanasoka wote waliokuwa wakiufuatilia mchezo huo.

SHUGHULI YA BONDENI IMEIVA.


Hatimae rimu 32 zitakazocheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 usiku wa kumakia leo zimefahamika miongoni mwa mashabiki wa soka ulimwenguini kote.

Michezo sita iliyokua inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki hao iliunguruma katika viwanja tofauti na mwishowe washindi walipatikana na kujiunga na mataifa 26 yaliyokua yameshafuzu kucheza fainali hizo.

Timu zilizofuzu usiku wa kuamkia leo ni pamoja na Algeria, Uruguay, Ufaransa, Slovenia, Ureno pamoja na Ugiriki.
orodha nzima ya timu 32 ni kama ifuatavyo;
AFRIKA.
ULAYA.

MAREKANI YA KATI NA KASKAZINI

Honduras (HON), Mexico (MEX) pamoja na USA (USA)

MAREKANI YA KUSINI;
OCEANIA;
MWENYEJI;

South Africa (RSA)

Wednesday, November 18, 2009

RONALDO KUWAWAHI BARCA ?


Kiungo mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ureno Cristiano Ronaldo huenda akaanza kufanya mazoezi na kikosi cha klabu yake ya Real Madrid siku ya ijumaa kufuatia kupona kwa kifundo cha mguu kilichokua kinamsumbua kwa muda mrefu.

Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Man Utd alipata maumivu ya kifundo cha mguu mnamo Sepetemba 30 kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya klabu ya Olympic Marseille.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na afisa wa klabu ya Real Madrid Emilio Butragueno zimeelza kuwa Ronaldo ataanza maozezi baada ya kufanyiwa vipimo jana na kuonekana yu fit kujiunga na wenzake kwa mara nyingine tena.

Roman Pavlyuchenko AKATA TAMAA.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Urusi Roman Pavlyuchenko amesema yu tayari kuondoka White Heart Lane kufuatia kuendelea kwa tatizo la kutojumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.


Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema kwa sasa maisha yamekuwa magumu, kufuatia utaratibu wa meneja wa Spurs Harry Redknapp ambao unamfaya kuwa chaguo la nne baada ya washambuliaji kama Robbie Keane, Jermain Defoe pamoja na Peter Crouch.

GATUSO NA FUNUNU ZA MAN CITY !!!!!!!!!


Wakala wa kiungo wa kimataifa toka nchini Italia na klabu ya AC Milan Gennaro Gattuso amekanusha taarifa za mchezaji wake kuwa mbioni kusajiliwa na klabu tajiri ya jijini Manchester inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza Manchester City.

Wakala wa kiungo huyo amekanusha taarifa hizo kufuatia kuwepo kwa uvumi ambao unadai kwamba kwa kipindi kirefu Gattuso hana furaha ya kuendenea kusalia huko San Siro hivyo yu radhi kuondoka katika ligi ya Sirie A na kujiunga na moja ya klabu inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwezi januari mwaka 2010.

SOTE TWASUBIRI NAFASI 32 KUJAZWA.


Nafasi sita pekee zasubiriwa kwa hamu kubwa kabl ya kipyenga hakijapulizwa Afrika kusini mwaka 2010.



MIDO YAJIPANGA KUREJEA.


Klabu ya Middlesbrough inayoshirikiu ligi daraja la kwana nchini Uingereza imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Stoke City Dave Kitson kwa mkopo wa miezi miwili.

kufuatia mafanikio hayo Kitson anakua mchezaji wa tatu kusajiliwa na Boro kwa mkopo tangu meneja Gordon Strachan alipochukua mikoba toka kwa Gareth Southgate.

Kitson huenda akacheza mechi yake ya kwanza mwishoni mwa juma hili hidi ya Nottingham Forest.

Wachezaji wengine waliosajiliwa klabuni hapo kwa mkopo ni pamoja na mshambuliaji Marcus Bent na kiungo Isaiah Osbourne.

Bent ameshapachika mabao mawili tu katika michezo 25 ya Ligi Kuu tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Reading mwaka 2008.

WENGER ATOA USHAURI.

Meneja wa klabu ya Arsenal ARSENE WENGER anaamini kiungo wa kimataifa Patrick Vieira anatakiwa kuchukua uamuzi wa kuondoka katika klabu yake ya sasa Inter Milan katika dirisha dogo la usajili endapo anahitajia kurejea kwenye klikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.

Arsene wenger amemshauri kiungo huyo kufanya hivyo huku akikanusha taarifa za yeye kuwa tayari kumrejesha kwenye kikosi chake kama ilivyozungumza siku kadhaa zilizopita.

Vieira mwenye umri wa miaka 33 amepoteza nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa baada ya kushindwa kupata nafasi ya kikosi cha kwanza chini ya kocha wa Inter Jose Mourinho.
Wenger amesema ili mchezaji aweze kucheza katika fainali za kombe la dunia lazima apate nafasi ya kucheza kila mara katika klabu yake hivyo ni vigumu kwa kiungo huyo kujihakikishia nafasi hiyo endapo Ufaransa itafanikiwa kushinda mchezo wake wa leo dhidi ya timu ya taifa ya Ireland ili iweze kucheza fainali za kombe la dunia.

Amesema endapo Viera atasikiliza ushauri wake kuna uwezekano mkubwa wa kucheza katika kombe la dunia za mwaka 2010.

Lakini alipoulizwa katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini Ufaransa kama anaweza kumrejesha kiungo huyo katika klabu ya Arsenal, Wenger amesema anaweza kucheza kamari kwa kuweka fedha kwa sababu hadhani kama Viera atarejea nchini Uingereza .

AKIONDOKA NAMI NAKWENDA.


Meneja wa klabu ya Liverpool RAFA BENITEZ amesema atakua tayari kuondoka Anfiled endapo klabu hiyo itaamua kumuuza mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando Torres.

Liverpool wapo kwenye mchakato wa kumuuza mshambuliaji huyo mwenye thamani kwa sasa kufuatia mzigo wa deni la paundi milioni 245 linalo waandama.

Benitez amesema iwapo wamiliki wa klabu hiyo ambao ni raia wa nchini Marekani watamzungunguka na kumuuza mshambuliji huyo hatoakubali kusalia Anfiled kwani atakua maehaibiwa mipango yake.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 49 amekuwa katika shinikizo kubwa msimu huu baada ya timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

FOSTER YU RADHI KUONDOKA.

Klabu ya Tottenham Hotspours inajipanga kumsajili mlinda mlango wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Manchester United Ben Foster kwa ada ya paundi milioni 6 ifikapo mwezi January mwaka 2010.

Kipa huyo wa Manchester United amekiri huenda akaihama klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford baada ya kuwa kipa wa tatu katika kikosi cha babu.

Tayari meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp ameshatangaza kuingia sokoni kwa lengo la kumsajili kipa mpya ambae atakua mbadala wa kipa wake namba mbili Carlo Cudicini aliepata ajali ya pikipiki juma lililopita .

Foster anafikiria uamuzi wa kuondoka Old Trafford ili aweze kujihakikishia nafasi ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki fainali za kombe la dunia nchini Afrika kusini mwaka 2010.

Foster mwenye umri wa miaka 26 alicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Brazil ambapo Uingereza walikubali kichapo cha bao moja kwa sifuri.

Monday, November 16, 2009

SULEIMAN AL-FAHIM AINGIA MIGUU YOTE.


Mwanahisa wa klabu ya Portsmouth Suleiman al-Fahim anaamini kuwa adhabu ya kutosajili mchezaji yoyote iliyoangushwa kwenye klabu hiyo itamalizika mapema juma hili.

Al Fahim, ambae aliuza asilimia 90 za hisa zake ambazo zilikua zinamfanya aimiliki klabu hiyo amesema utaratibu wa kuamini adhabu hiyo itamalizika juma hili, utatoa mustakabali wa kufahamu The Pompey watamsajili mchezaji yupi wakati wa usajili mwezi januari mwaka 2010.

Portsmouth walitakiwa kutosajili mchezaji yoyote mpaka hapo watakapolipa mzigo wa madeni unaowaandama kwa sasa.

NGOMA YAPELEKWA SUDAN.


Baada ya kufanya kweli kwa ushindi wa mabao mawili kwa sifuri mwishoni mwa juma lililopita timu ya taifa ya Misri inatarajia kucheza mchezo wa mtoano nchini Sudan dhidi ya timu ya Algeria kwenye mchezo wa kuwani nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2010.

Mchezo huo utakaochezwa katika uwanja huru unatarajiwa kupigwa siku ya jumatano hatua ambayo itawalazimu na mashabiki wa nchi hizo kusogea huko nchini Sudan kuzishangilia timu zao.

Kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa sifuri walioupata Misri ulizifanya timu hizo kuwa sawa katika kila hali hatua ambayo imelilazimu shirikisho la soka duniani FIFA kuamuru mchezo huo uchezwe kwenye uwanja huru ili kumpata yule atakaelekea bondeni mwa bara la Afrika mwaka 2010.

George Burley KIKAANGONI.


Kamati ya utendaji ya chama cha soka nchini Scotland *Scottish Football Association* inatarajia kukutana na kujadili mustakabali wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo George Burley.


Kikao hicho kinatarajiwa kutoa jibu sahihi kwa kocha huyo kama ataendelea kubaki na kazi yake ama la, hasa baada ya timu ya taifa ya Scotland kukosa nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2010.


Burley alionekana kushindwa kuipeleka kwenye hatua ya mchezo wa mtoano timu ya taifa ya Scotland baada ya kukubali kichapo cha mabao matatu kwa sifuri toka kwa timu ya taifa ya Wales.

Sunday, November 15, 2009

ENKE ATAENDELEA KUKUMBUKWA DAIMA.

Maelfu ya watu wamehudhuria ibada ya aliekuwa kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani pamoja na klabu ya Hannover 96, Robert Enke aliefariki kati kati ya juma hili.

Ibada hiyo imefanyika katika uwanja wa mpira uliopo kaskazini wa Hanover.

Wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa waliongoza katika kutoa risala za kumkumbuka ya kipa huyo ambae alifikwa na umauti baada ya kugongwa na treni hali mbayo iliwashangaza wengi nchini Ujerumani pamoja na duniani kote.

Mke wa marehemu ameeleza kwamba Enke aliishi kwa muda mrefu katika hali ya unyonge, kabla ya kuamua kujirusha mbele ya treni iliyokuwa katika mwendo wa kasi.



AJALI + Carlo Cudicini = MAJUMA 12


Kipa wa klabu ya Tottenham Carlo Cudicini anaendelea vyema na ameonyesha dalili nzuri za kupona majeraha yake aliyoyapata kwenye ajali kati kati ya juma lililopita.


Kipa huyo pamoja na kuonyesha dalili njema za kupona itamlazimu kuwa nje ya uwanja wa muda wa majuma 12 ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida.


Carlo Cudicini mwenye umri wa miaka 36 alipata ajali baada ya pikipiki yake aina ya BMW kugongana na gari aina ya Ford Fiesta ambalo lilikua likiendeshwa mwana mama.

BENITEZ AELEKEZA MACHO EMIRATES.


Benchi la ufundi la klabu ya Liverpool limeonyesha kuwa tayari kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Croatia na klabu ya Arsenal Eduardo da Silva.


Liverpool wameonyesha hatua hiyo kufuatia taarifa zinazodai kwamba mshambuliaji huyo kwa sasa hana raha huko Ashburton Grove kufuatia hatua finyu zinazo onekana za kutopewa mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal.


Meneja wa klabu ya Liverpool Rafa Benitez tayari ameshaandaa kitita cha paund million 10 ambacho kitatumika kama ada ya uhamisho wa Eduardo ambae huenda kapewa nafasi ya kusaidiana na David Ngog, katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

NDOTO ZA MDACHI ZAYEYUKA.


Hofu imetanda kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal kufuatia mshambuliaji wao tegemezi kwa sasa Robin van Persie kuumia kwenye mchezo wa jana wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu yake ya taifa ya Uholanzi dhidi ya timu ya taifa ya Italia.

Mshambuliaji huyo ameumizwa kifundo cha mguu na yasemekana huenda akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya siku thelathini hilo limethibitishwa na kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Bert van Marwijk.

Kufuatia hali hiyo ndoto za Van Parsie kucheza mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Man City inapotea na itamlazimu kuwa mtazamaji wa timu ya vijana ya Arsenal ambayo inatarajiwa kucheza kwenye pambano hilo la Disemba mosi.

NI KWELI ATAREJEA?


Aliyekua meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amekiri kwamba huenda akarejea nchini uingereza kufanya kazi na pengine akamiliza muda wake wa kufundisha soka akiwa nchini humo .

Mourinho ambaye kwa sasa ni meneja wa klabu ya Inter Milan, kwa muda sasa amewakosesha raha mashabiki wa soka nchini Uingereza kutokana na msimamo wake na mafanikio aliyoyapata baada ya kuwasili Stamford Bridge mwezi September 2007 akishinda mataji mawili mfululizo ya ligi ya Premier na kombe la FA Cup na mataji mawili ya Carling.


Mourhino aliweza kujizolea mashabiki wengi kwa muda wa miaka mitatu na nusu aliyokaa nchini Uingereza na baada ya kuhamia nchini Italia ameendeleza mafanikio yake kwa kushinda taji la Scudeto katika ligi kuu ya soka nchini Italia maarufu kama Serie A.


Taarifa zinaeleza kuwa huenda Mourinho akachukua nafasi ya Sir Alex Ferguson atakapostaafu kuifundisha klabu ya Manchester United.

CARLOS ASHANGAZA!!!!!!!!!!


Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Carlos Tevez amesema anatarajia kustaafu kucheza soka iwapo timu ya taifa ya Argentina itafanikiwa kushinda kombe la dunia kwa sababu ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza huku pia akiwa amechoka kutokana na kucheza sana soka.

Tevez mwenye umri wa miaka 25 amesema muda wake kuichezea timu yake ya taifa umepita baada ya kushindwa kufanya vizuri katika kampeni za kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia.


Pia Tevez amesema kwa sasa wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina hawathaminiwi na mashabiki na wadau wa soka nchini humo kwa madai kwamba wachezaji hao wanathamini pesa badala ya bendera.

Friday, November 13, 2009

AJALI MATEMBEZINI.


Mlinda mlango wa klabu ya Tottenham Hotspur Carlo Cudicini amepata maumivu makali mwilini mwake baada ya kupata ajali na pikipiki mashariki mwa jiji la London .

Cudicini amepata ajali hiyo baada ya pikipiki yake aina ya BMW kugongana uso kwa uso na gari ndogo na kupata maumivu mkononi na kiunoni ambapo bado taarifa za vipimo zinasubiriwa na uongozi wa klabu hiyo kutoka hospitalini alikolazwa.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 36 alisajiliwa Spurs akitoka kwa mahasimu wao klabu ya Chelsea mwezi January mwaka huu kama mchezaji huru na tayari ameshacheza mechi 8 wakati kipa namba moja wa klabu hiyo Heurelho Gomes alipokuwa majeruhi .

Cudicini aliichezea klabu ya Chelsea kwa muda wa miaka 10 na pia amewahi kuzichezea klabu za AC Milan na Lazio za nchini kwao Italia.

Dereva wa gari lililogongana na pikipiki ya kipa huyo akikuwa mwanamke na kwa bahati nzuri yeye hakuumia pamoja na mwanae aliekua nae.

NANI ACHOSHWA NA TABIA ZA BABU.

Winga wa kimataifa toka nchini Ureno anayeichezea klabu ya Manchester United NANI amepinga mfumo unaotumiwa na meneja wake Sir Alex Ferguson kuwaongoza wachezaji wake.

Winga huyo ambae anaonekana kushindwa kuziba pengo la anayeonakana Cristiano Ronaldo huenda akawa amajipalia makaa ya kuendelea kusalia Old Traford yalipo makao makuu ya klabu ya Man utd.

Akihojiwa na gazeti moja la huko nchini Ureno Nani amesema meneja huyo hajatimiza ahadi zake alizomuahidi ikiwa ni pamoja na kumuondoa kabisa katika kikosi cha kwanza hatua ambayo imepelekea kiwango chake kushuka siku hadi siku.

Nani amesema Ferguson ni mtu ambaye hatabiriki na asieleweka hivyo ana wakati mgumu kutumiza matarajio ya mashabiki wake kutokana na kutopata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu uwanjani na hivyo kushindwa kufunga mabao.

Amesema mara nyingi akipata nafasi anacheza vizuri lakini amekuwa hana uhakika wa kupata nafasi katika mchezo ujao hali ambayo inamkatisha tamaa.

Amesema hakuota kuwa na bahati ya kucheza mechezo mikubwa dhidi ya klabu za Liverpool, Manchester City na Tottenham, mechi ambazo zinamjengea mchezaji uwezo ambapo mpaka sasa kwake binafsi ameshacheza michezo 13 na kufunga bao moja.

Akizungumzia tabia za meneja huyo Nani amesema Sir Alex Ferguson hana simile hasa pale anapoamua kumsema mchezaji mbele ya wachezaji wenzake tena kwa sauti bila hata kujali hata wachezaji wakongwe kama vile Ryan Giggs na Gary Neville ambao mara nyingi wamekuwa wakilaumiwa na kutukanwa.

Hatua hii ya Nani kumzungumzia meneja wake huenda ikahitimisha uwepo wake katika klabu hiyo hasa baadhi ya wachezaji waliwahi kudiriki kwenda kinyume na matakwa ya Ferguson ambao waliishia kuihama klabu hiyo.

Itakumbukwa kwamba beki wa kimataifa toka nchini Uholanzi aliyestaafu soka kwa sasa Jaap Stam aliwahi kuchapisha kitabu chake mwaka 2001 kilichukua kinazungumzia maisha yake ya soka na kumlaumu Ferguson ambaye aliamua kumuuza katika klabu ya Lazio kwa paundi milioni 16.5.

Miaka miwili baadaye , David Beckham aliuzwa katika klabu ya Real Madrid baada ya kukorofishana na meneja huyo.

Mwezi Novemba mwaka 2005 ilikuwa ni zamu ya Roy Keane aliyejiunga na klabu ya Celtic kwa miezi sita ya maisha yake ya kucheza soka yaliyokuwa yamesalia baada ya kujibishana na meneja huyo kutokana na kutoridhidhwa na uwezo wa timu hiyo katika kipindi hicho.

Hatua hiyo ya Nani huenda ikahitimisha ndoto zake za kurithi nafasi ya Mreno mwenzake Ronaldo aliyehamia katika klabu ya Real Madrid miezi minne na nusu iliyopita baada ya kutumainiwa na wengi kwamba angeweza kuziba pengo hilo kutoka na kushabihana kiuchezaji.


Nani ambaye alisajiliwa na Ferguson kutoka klabu ya Sporting Lisbon mwezi July 2007 kwa ada ya paundi milioni 16 amesema pamoja na kuzungumza yote yaliyo moyoni mwake kuhusu Sir Alex Ferguson bado hana mpango wa kuihama klabu hiyo hivyo kinachosubiriwa ni hatua ambayo itachukuliwa na na babu.

KILA NCHI NA SHERIA ZAKE !!!!!!!!!


Mshambuliaji nyota wa kimataifa toka nchini Nigeria Stephen Worgu anayecheza soka la kulipwa nchini Sudan amekuhumiwa kuchapwa viboko na kulipa fainai baada ya kukutwa na hatia ya kunywa pombe na kuendesha gari.

Worgu ambaye anaichezea klabu ya Al Merreikh amekutwa na kosa hilo ambalo ni kubwa huko kaskazini ya Sudan tofauti na ilivyo huko Kusini mwa Sudan ambapo waumini wa dini ya Kiislam ni wachache.

Hata hivyo adhabu hiyo bado haijatekelezwa kufuatia wakili wa mchezaji huyo kukata rufaa iwapo atashindwa rufaa hiyo Worgu atatakiwa kuchapwa viboko 40 na kulipa faini ya paundi za Sudan 250 sawa na dola 100 za Marekani .

Paundi 50 itakuwa ni kwa ajili ya kunywa pombe na paundi 200 kwa ajili ya kuendesha gari akiwa amelewa.

Itakumbukwa kwamba Worgu alisajiliwa na klabu ya Al Merreikh kwa uhamisho wa ada ya dola za kimarekani milioni 2.6 akitokea katika klabu ya Enyimba ya Nigeria,uhamisho ambao ni wa ghali katika historia barani Afrika .

Worgu alikuwa mfungaji bora katika ligi ya klabu bingwa barani Afrika mwaka 2008 kwa kufunga mabao 13 lakini tangu alipohamia nchini Sudan kiwango chake kimeshuka.

Thursday, November 12, 2009

ARSENAL YANYATIA KINDA JINGINE.


Washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal wanaendelea na taratibu zao za kutaka kumsajili winga wa kimataifa toka nchini Israel na klabu ya Fc Barcelona Gai Yigaal Assulin.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 18 tayari ameshakataa kujiunga na klabu ya Chelsea mnamo mwaka 2007, na huenda akasaini mkartaba wa kuendelea kusalia huko Nou Camp.


Kwa muda mrefu sasa klabu ya Arsenal imekuwa na mpango wa kuwasajili wachezaji chipukizi na huo umeonekana kuwa mfumo wa meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger.