


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Adebayor usiku wa kuamkia leo amekamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Man City.
Man City wamekamilisha usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa ada ya uhamisho wa paund milion 25 akitokea kaskazini mwa jiji la London yalipo makao makuu ya klabu ilitokuw ainammiliki ya Arsenal.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukamilisha usajili huo, Emmanuel Adebayor amesema ameelekea City Of Manchester kwa lengo la kujitengenea historia mpya ya maisha yake ya soka pamoja kuiweka Man City katika hadhi ya kiushindani.
Adebayor amesema mara kadhaa amekuwa akitaka kujiwekea historia ya maisha yake katika mchezo huo ambapo pamoja na kufanya hivyo akiwa na vilabu vingine pamoja na timu yake ya taifa, bado anatamani kuendelea kufanya hivyo akiwa na klabu yake mpya ya Man City.
Nae meneja wa klabu ya Man City Mark Hughes amesema ana hakika kuwasili kwa Emmanuel Adebayor katika kikosi chake ni ishara tosha ya kuendelea kumaliza tatizo la ukame wa mabao uliokuwa unakisumbua kikosi chake hivyo ana imani mshambuliaji huyo atamaliza tatizo hilo.
Ikumbukwe kuwa Emmanuel Adebayor kabla ya kujiunga na klabu ya Arsenal mnamo mwaka 2006 alikuwa anaitumikia klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa.
Kusajiliwa kwa Emmanuel Adebayor kunaifanya klabu ya Man City kuendelea kuwa na mchakato wa kutaka kuiimarisha safu yake ya usahambuliaji ambayo kwa sasa ina wachezaji kama Carlos Tevez, Roque Santa Cruz, Robinho, Craig Bellamy pamoja na Benjani Mwaruwari.
Usajili huyo wa wachezaji hao ambao tayari wameshawika wakia na vilabu vingine umepea nguvu na mmiliki wa Man City Sheikh Mansour bin Zayed al Nahyan ambae amepania kuleta mapinduzi ya soka nchini Uingereza na kubadilisha taswira ya mtazamo wa nafasi nne za juu za ligi hiyo ambao mara kadhaa umekuwa haubadiliki.
Katika kipindi hiki cha usajili Adebayor anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na klabu hiyo ambayo tayari imeshawapata akina, Santa Cruz Gareth Barry, pamoja na Carlos Teves.
Kikubwa mbacho hakitasahaulika kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal dhidi ya mshambuliaji huyo ni ile hatua yake ya kupachika mabao 30 ndani ya michezo 48 aliyocheza katika masimu wa mwkaa 2007-08.
Mkubwa kwanza nikiri wazi kuwa mimi ni Arsenal damu ila kwa Adebayor kuondoka ni sawa kabisa, msimu uliopita hakuwa na manufaa kwetu, alikuwa anapewa pasi kumi za wazi za kufunga ila alishindwa, sasa tulishamchoka yeye na Betneir, hawana maana kabisa, natumai umeona kazi ya Ashvin siku ya Liverpool ni soo, sasa Arsenal tunahitaji wachezaji kama Ashvin sio wajingawajinga kama Adebayo na Betiner
ReplyDeleteMr Sam Mbilu
SUA Morogoro