KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, August 11, 2009

MR ABRAMOVICH AMFUNGIA SAFARI RIBERY.


Kibopa wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich anatarajia kuruka na ndege hii leo kuelekea nchini ujerumani kwa ajili ya kufanya tarartibu za kuongeza ofa ya paund million 40 ambazo anaamini zitaweza kumsajili winga wa kimataifa toka nchini Ufaransa na klabu ya Bayern Munich Franck Ribery.

Kibopa huyo anaelekea nchini humo baada ya kuzungumza kwa njia ya simu na meneja mkuu wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness juma lililopita.

Mmoja wa viongozi wa klabu ya Bayern Munich ameleeza kuwa kufuatia simu iliyopigwa na Mr Abramovich Uli alishushwa na yale aliyoelezwa.

Hata hivyo meneja mkuu wa klabu ya Bayern Munich amekubalia kukutana na kibopa huyo na ndio maana hii leo ameifunga safari kuelekea huko nchini Ujerumani.

No comments:

Post a Comment