
Kiungo wa pembeni wa kimataifa toka nchini Ureno na klabu ya Man Utd Luís Carlos Almeida da Cunha Nani ataikosa michezo ya mwanzo ya msimu wa ligi kufuatia maulivu ya bega yanayomkabili.
Kiungo huyo anakabiliwa na maumivu hayo aliyoyapata kwenye mchezo wa kuwania ngao ya hisani dhidi ya Chelsea uliounguruma August 09 kwenye uwanja wa Wembley na kushuhudia The Blues wakitawazwa kuwa mabingwa wa ngao hiyo.
Luís Carlos Almeida da Cunha Nani, ambae alipachika bao la kwanza katika mchezo huo alilazimika kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na winga wa kimataifa toka nchini Ecuador Antonio Valencia katika dakika ya 60.
No comments:
Post a Comment