KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 8, 2009

STOPER NEMANJA AUMIA.

Beki wa klabu ya MANCHESTER UNITED Nemanja Vidic atakuwa nje ya uwanja uwanja kwa muda w amajuma mawili kufuatia majereaha yanayomkabili.

Meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson amethibitisha kuwa beki huyo wa kimataifa toka nchini Serbia atakosa michezo miwili ambayo ni ngao ya hisani dhidi ya klabu ya Chelsea utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Wimbley na mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Birmingham.


Pia katika mchezo wa ngao ya hisani Fergie huenda wakawakosa mabeki wake wengine ambao ni Wes Brown na Gary Neville, ambapo hata hivyo kuna matumaini makubwa Brown akaonekana katika mchezo huo.



Katika hatua nyingine meneja huyo amesisitiza kwamba mshambuliaji Michael Owen atafunga magoli mengi msimu ujao licha ya mashabiki wenginulimwenguni kumbeza.

Ferguson ametoa kauli hiyo baada ya Owen kukosa mabao mengi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya klabu ya Valenchi ambapo mchezo huo ulimalizika kwa kushuhudia mashetani wekundu wakiibuka na ushindi wa mbao mawili kwa sifuri.

Fergie amesema pamoja na mshambuliaji huyo kufikia hatua ya kutopata nafasi ya kucheza soka katika kiwango cha juu ana matumaini Owen atashawishiwa hali ya uchezeshaji wa kiungo wa klabu hiyo Paul Scholes aliyereja dimbani baada ya kuumia na kufanikiwa kuwa katika kiwango cha juu hatua iliyomfanikisha kucheza fainali ya kombe la klabu bingwa barani ulaya akiwa na umri wa miaka 34.



Amesema hana wasiwasi wowote na Owen hasa baada ya kumuona Scholes anarejea uwanjani mara baada ya kuumia mara kadha .




No comments:

Post a Comment