Aliyekuwa meneja wa klabu ya Chelsea, Avram Grant ametangazwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Portsmouth inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Avram Grant ametangazwa kushika wadhifa huo, baada ya kutimuliwa kwa Paul Hart ambae alishindwa kukiongoza vyema kikosi cha klabu hiyo toka mwanzoni mwa msimu huu.
Avram Grant ametangazwa kushika wadhifa huo, baada ya kutimuliwa kwa Paul Hart ambae alishindwa kukiongoza vyema kikosi cha klabu hiyo toka mwanzoni mwa msimu huu.
Hii ni mara ya pili kwa Grant kufanya kazi kwenye klabu hiyo ya kusini mwa nchini Uingereza ambapo kwa mara ya kwanza alifanya kazi kama mkurugenzi wa soka.
Grant ataanza kazi mwishoni mwa juma hili ambapo kikosi chake kitakuwa na changamoto kubwa ya kuwakabili Manchester Utd kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment