KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 8, 2009

BULLARD NJE TENA.


Kiungo wa kutumainiwa wa klabu ya Hull City Jimmy Bullard atakua nje kwa muda wa majuma sita hadi manane yajayo hatoweza kucheza kwa wiki sita hadi nane baada ya kuumia goti.

Bullard alifanyiwa uchunguzi wa goti lake la kushoto usiku wa Jumatatu lakini klabu yake ya Hull haijaeleza ni kwa kiwango gani ameumia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliumia alipoanguka vibaya mwishoni mwa juma lililopita kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Aston Villa.

Mapema mwaka huu kiungo huyo hakucheza kwa muda wa miezi tisa baada ya kuumia goti lake la upande wa kulia, lakini baada ya kupona na kurejea kwake uwanjani kulimfanya achaguliwe mchezaji bora wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza mwezi wa Novemba.

No comments:

Post a Comment