KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 17, 2009

WENGER ASOMA UPEPO WA RAMANI.


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amekilaumu chama cha soka nchini Uingereza kufautia ratiba ya ligi kuu namna ilivyopangwa.

Wenger ametoa malalamiko hayo baada ya mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya klabu ya Burnley ambao umemalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Wenger amesema Arsenal mchezo ujao wa ligi wanacheza na klabu ya Hull City ambayo haijacheza mchezo wowote toka disemba 12.

Wenger amesema kutokana na utaratibu huo anahofia huenda wachezaji wake wamechoka kutokana na kucheza michezo miwili mfululizo mwishoni mwa juma lililopita pamoja na kati kati ya juma hili.

No comments:

Post a Comment