KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 20, 2010

BLANC KOCHA MPYA UFARANSA.


Shirikisho la soka nchini Ufaransa FFF hatimae limefanikiwa kuushawishi uongozi wa klabu ya Bordeaux juu ya kumuachia meneja wao Laurent Blanc aliekua anapewa nafasi kubwa ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa hilo mara baada ya fainali za kombe la dunia huko nchini Afrika kuisni.

Makubaliano hayo sasa yanampa nafasi Blanc kushika pahala pa kocha wa sasa wa timu ya taifa ya Ufaransa Raymond Domenech mara baada ya fainali za kombe la dunia zitakazoanza June 11 - July 11 mwaka huu.

Blank mwenye umri wa miaka 44 amefanikiwa kupewa nafasi hiyo kufuatia kuwa na sifa za kutosha ambazo ziliipelekea klabu yake kufanya vyema kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu baada ya kufika kwenye hatua ya robo fainali.

Hata hivyo dalili za Black kukubaliwa na uongozi wake kukinoa kikosi cha Ufaransa zilianza kuonekana mwishoni mwa juma lililopita baada ya uongozi wa Bordeaux kumtakia kila la kheri kule alipotarajia kuelekea mara baada ya kufanya vyema msimu huu.

Nao viongozi wa shirikisho la soka nchini Ufaransa wakiongozwa raisi wao Jacques Lambert wameushukurua uongozi wa klabu ya Bordeaux kwa kukubalia ombi lao kiungwana ambalo lina manufaa katika taifa la nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment