Fainali za mataifa ya bara la afrika chini ya umri wa miaka 17, hii leo zimefikia tamati kwa kushuhudia mchezo wa hatua ya fainali ukiunguruma kwenye uwanja wa Amahoro uliopo mjini Kigali nchini Rwanda kati ya wenyeji dhidi ya Burkina Faso.
Mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi wa Rwanda wakiongozwa na raisi wao Paul Kagame umemalizika vyema kwa timu ya Burkina Faso kutawazwa kuwa mabingwa wa fainali hizo za mwaka 2011 ambazo ni fainali za tisa toka zilipoanzishwa mwaka 1995 kule nchini Mali.
Burkina Faso wametawazwa kuwa mabingwa wa fainali hizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Zaniou Sana katika dakika ya 56 pamoja na Abdou Aziz Kabore katika dakika ya 71 huku Charles Tibingana Mwesigye akiifungia bao pekee Rwanda.
Kumalizika kwa fainali hizo za barani|Afrika chini ya umri wa miaka 17, kumetafsiriwa kama sehemu ya kuanza kwa maandalizi ya fainali za kombe la dunia za vijana chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika nchini Mexico mwezi July ambapo bara la Afrika litawakilishwa na nchi za Burkina Faso, Rwanda, Ivory Coast pamoja na Congo Brazzaville.
No comments:
Post a Comment