KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, February 17, 2011

GATUSO ALIWAAMBIWA YEYE NI KAHABA WA KIUME.


Wakala wa kiungo wa kimataifa toka nchini Italia pamoja na nahodha wa klabu ya AC Milan Gennaro Ivan Rino Gattuso amemtetea mchezaji wake kwa kusema alitukanwa kabla ya kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa siku ya jumanne dhidi ya Spurs huko mjini Milan.

Wakala wa kiungo huyo ameliweka hadharani suala hilo alipohojiwa kwenye moja ya vipindi vya Radio Kiss Kiss iliopo mjini Napoli nchini Italia mbapo amesema amezungumza na mchezaji wake na amemueleza kwamba meneja msaidizi wa klabu ya Tottenham Joe Jordan alimtusi na yeye kwa hasira alijikuta akifanya vitendo vya utovu wa nidhamu.

Wakala huyo amesema endapo Joe Jordan asingemtamkia Gatuso maneno machafu katu zogo lililojitokeza wakati wa mchezao ukiendelea na baada ya kumalizika lisingejitokeza kwa kudai anamfahamu mchezaji wake kutokana na tabia aliyo nayo.

Amedai kwamba Joe Jordan alimwambia Gatuso yeye ni Kahaba wa kiume wa kitaliano anaejiuza na kauli hiyo aliitoa mara baada ya kiungo huyo kumchezea ovyo mshambuliaji Peter Crouch.

Kama itakumbukwa vyema Gatuso alipoulizwa juu ya suala hilo mara baada ya mchezo kumalizika alidai walikua wakizungumza na Joe Jordan lugha ya kiscotish na alipotakiwa aseme ni nini walichokua wakiambiana aligoma kata kata kuelezea.

Tayari kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA imeshatangaza kukutana mwanzoni mwa juma lijalo kujadili kesi hiyo .

No comments:

Post a Comment