KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, September 30, 2011

SIKUSTAHILI KUFANYA VILE.

Siku mbili kabla ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambao utawakutanisha mahasimu wa kaskazini mwa jiji hilo, Tottenham Hotspurs dhidi ya Arsenal, mshambuliaji aliesajiliwa kwa mkopo huko White Hart Lane akitokea Man City Emmanuel Sheyi Adebayor, ametamba kuifunga The Gunners katika mchezo huo.

Adebayor ametamba kuifunga Arsenal katika mpambano huo wa siku ya jumapili, huku akiringia utaratibu mzuri alioanza nao mara baada ya kusajiliwa klabuni hapo, ambapo alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza akiwa na Spurs katika mchezo dhidi ya Wolves.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Togo, amesema anaamini mchezo huo utakua mgumu kutokana na historia ya vikosi vya klabu hizo vinapokuatana, lakini atajitahidi kadri awezavyo, kuhakikisha anafanya mipango ya kuwanyanyua mashabiki wa Tottenham ambao tayari wameshamkubali kufuatai kazi nzuri aliyoifanya.

Hata hivyo Adebayor amekiri alifanya makosa pale aliposhangilia mbele ya mashabiki wa Arsenal baada ya kufunga bao dhidi ya klabu hiyo ambayo ilimuuza Man City kwa ada ya uhamisho wa paund million 25.

Nae meneja wa Spurs Harry Redknapp amesema wanakwenda katika mchezo huo wa jumapili huku wakiamini Arsenal ni wazuri na wala hawatowadharau kutokana na misukosuko iliyowapata siku za hivi karibuni.

Amesema anatambua umuhimu wa mchezo huo, na katu hawezi kujidaia matokeo ya michezo ya ligi ya msimu uliopita ambapo Spurs waliibuka na point nne baada ya kupata ushindi emirates stadium na kulazimisha sare white hart lane.

No comments:

Post a Comment