KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, October 4, 2011

Roman Abramovich APANIA KUIHAMISHA CHELSEA.

Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amedhamiria kubadilisha historia ya klabu hiyo baada ya miaka 106 kupitia, kwa kuhamisha makazi kutoka Stamford Bridge hadi katika eneo lingine huko mjini London nchini Uingereza.

Roman Abramovich alikua na matarajio ya kuuendeleza uwanja wa Stamforde Bridge kwa kuubomoa na kuutengeneza upya lakini utaratibu huo umepiga hatua na kufikiria kununua sehemu nyingine kwa ajili ya kujenga uwanja mpya ambao utakua chachu ya kupata makazi mapya ya klabu hiyo.

Tayari kibopa huyo ameshanunua sehemu ambayo ni karibu wa uwanja wa sasa, na endapo dhana ya kujenga uwanja mpya itakamilika basi Chelsea wataingai kati utaratibu wa kuwa miongoni mwa vilabu vitakavyomiliki uwanja utakaokuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki elfu 60.

Hata hivyo ifahamike kwamba kwa sasa Roman Abramovich hana sauti ya umiliki wa uwanja wa Stamford Bridge, zaidi ya kuomba namna ya kununua hisa kutoka kwa mashabiki wa Chelsea wenye haki ya umiliki baada ya kufanya maboresho miaka 14 iliyopita.

Kutokana na hali hiyo Roman Abramovich ametoa offer ya paundi milioni 10 ili kulipa fidia ya hisa za mashabiki na pia yu tayari kulipa sehemu ya mkopo wanaodaiwa mashabiki hao wa paundi milioni 8.5 ambao ulitumika wakati wa kufanyika kwa marekebisho ya uwanja wa Stamforde Bridge.

Kwa upande wa mwenyekiti wa klabu hiyo Bruce Buck amesema ana imani wanahisa wa Chelsea watakubaliana na andiko hilo la Roman Abramovich.

4 comments: