







Klabu ya Chelsea imefanikiwa kutwaa ngao ya hisani baada ya kuwachabanga Man Utd kwa changamoto wa penati nne kwa moja.
Klabu hizo zilifikia hatua ya kupigiana penati baada ya kutoshana nguvu ndani ya dakika 90 kufuatia mabao mawili yaliyofungwa na Ricaldo Cavalho pamoja na Lampard kwa upande wa Chelsea huku, Luís Carlos Almeida da Cunha NANI na Rooney wakifunga kwa upande wa Man Utd.
Katika hatua ya Mikwaju ya panati, kwa upande wa Chelsea wapigaji walikuwa ni Frank Lampard, Michael Ballack, Didier Drogba pamoja na Solomon Kalou ambao wote walipata.
Kwa upande wa Man utd Michael Carick ndie alipata mkwaju pekee, huku Ryan Giggs, na Patrice Evra wakikosa mikwaju yao.
Hongela watoto wa the blue.
ReplyDeleteBila shaka mmetuanzia msimu mpya vizuli.bila shaka huu mwaka mtatufurahisha sisi washabiki wenu vyakutosha.