Sunday, August 9, 2009

CHELSEA MABINGWA WA NGAO YA HISANI;

shamra shamra kabla ya mchezo wa ngao ya hisani.
Wachezaji wa klabu ya Man utd pamoja na Chelsea wakiombeleza kabla ya mchezo kuanza, kufuatia kifo cha Sir Bobby Robson.

Luís Carlos Almeida da Cunha Nani akishangilia bao la kwanza aliloifungua klabu yake ya Man Utd.

Bao la kusawazisha la Chelsea likifungwa na Ricaldo Cavalho

Bao la pili la Chelsea likifungwa na Frank Lampard.

Bao la pili la kusawazisha la Man Utd likifungwa na Wyne Rooney

Solomon Kalou akipachika mkwaju wa penati wa mwisho ambao umeipa ushindi Chelsea.


Klabu ya Chelsea imefanikiwa kutwaa ngao ya hisani baada ya kuwachabanga Man Utd kwa changamoto wa penati nne kwa moja.

Klabu hizo zilifikia hatua ya kupigiana penati baada ya kutoshana nguvu ndani ya dakika 90 kufuatia mabao mawili yaliyofungwa na Ricaldo Cavalho pamoja na Lampard kwa upande wa Chelsea huku, Luís Carlos Almeida da Cunha NANI na Rooney wakifunga kwa upande wa Man Utd.

Katika hatua ya Mikwaju ya panati, kwa upande wa Chelsea wapigaji walikuwa ni Frank Lampard, Michael Ballack, Didier Drogba pamoja na Solomon Kalou ambao wote walipata.
Kwa upande wa Man utd Michael Carick ndie alipata mkwaju pekee, huku Ryan Giggs, na Patrice Evra wakikosa mikwaju yao.


1 comment:

  1. Hongela watoto wa the blue.
    Bila shaka mmetuanzia msimu mpya vizuli.bila shaka huu mwaka mtatufurahisha sisi washabiki wenu vyakutosha.

    ReplyDelete