Thursday, August 6, 2009

DAVID BECKHAM KUREJEA MAN UTD.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza DAVID BECKHAM huenda akarejea katika klabu yake ya zamani ya Manchester United baada ya kustaafu soka.

Nyota huyo wa zamani wa mashetani wekundu anafikiriwa kuwa balozi baada ya wamiliki wa klabu hiyo kuwa katika harakati ya kuiimarisha klabu hiyo sokoni katika maeneo mbalimbali duniani kote.

Nyota huyo wa zamani wa klabu hiyo alikosana na meneja wake Alex Ferguson miaka saba iliyopita na kupelekea hatua ya kuondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Real Madrid.
Beckham anatarajia kutumika kulitangaza jina la klabu hiyo ili kuvutia wawekezaji wanaoweza kufanya biashara na Man Utd hususani kwenye nchi za mashariki ya mbali.

Taarifa toka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa licha ya suala kuonekana kama ni fununu lakini bado wengi wanaamini kwamba Beckham ataendelea kuwa mwanafamilia wa Manchester United.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa Beckham anaweza kufanya kile ambacho Sir Bobby Charlton alichokifanya kwa muda wa miaka mingi.

Hata hivyo inasemekana Fergie amekuwa akiwashinikiza wamiliki wa klabu hiyo familia ya Glazer kuwa na mahusiano na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo.

Aidha taarifa kutoka ndani ya Old Trafford zinaeleza kuwa baada ya klabu hiyo kumuuza Cristiano Ronaldo aliyekuwa alama ya biashara, huenda Becks akasaidia kuziba nafasi hiyo baada ya kustaafu kucheza soka.

Pia inasemekana hata meneja Ferguson anaweza kuwa balozi wa klabu hiyo atakapofikia hatua ya kustaafu.




No comments:

Post a Comment