Uongozi wa klabu ya Zenit St Petersburg ya nchini Urusi amemtimua kazi meneja wao Dick Advocaat kufuatia matokeo mabovu yanayoikabili klabu yao kwa sasa.
Kutimuliwa kwa meneja huyo mwenye umri wa miaka 61 huenda kukawa doa katika taratibu zake za kutaka kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji ambapo mpango huo alikuwa ameupanga mara baada ya msimu huu kumalizika.
Advocaat alianza kuinoa klabu ya Zenit St Petersburg mnamo mwaka 2006 na aliiwezesha kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho la soka barani Ulaya *UEFA CUP* mnamo mwaka 2008 baada ya kikosi chake kukibanjua kikosi cha klabu ya Rangers mabao mawili kwa sifuri.

No comments:
Post a Comment