KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, August 8, 2009

HABIB BEYE AREJEA LIGI KUU.


Klabu ya Aston Villa imekamilisha taratibu wa kumsajili beki wa kimataifa toka nchni Senegal Habib Beye.

Beki huyo amesajiliwa na klabu hiyo ya mjini Birmingham na tayari ameshasaini mkataba wa miaka mitatu huku ada yake ya usajili ikifanywa kuwa siri kufuatia makubaliano yaliyoafikiwa na uongozi pande zote mbili.

Habib Beye amekamilisha dili hilo, ambalo linamrejesha katika timbwili timbwili la ligi kuu ya soka nchini Uingereza baada ya klabu yake ya zamani ya Newcastle Utd kushuka daraja msimu uliopita.

Kukamilika kwa usajili huo kunamfanya Habib Beye mwenye umri wa miaka 31, kuungana na wachezaji wengine waliojiunga na klabu ya Aston Villa katika kipindi hiki cha usajili ambao ni Stewart Downing pamoja na Fabian Delph.


No comments:

Post a Comment