KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Sunday, August 9, 2009

HUGHES "SINA WASI WASI".


Meneja wa klabu ya Man City Mark Hughes amesema hana wasi wasi na beki wake wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Habib Kolo Toure ambae jana aliumia kwenye mchezo wa kujipima ubavu dhidi ya klabu ya Celtic ya nchini Scotland.

Hughes amesema kuiumia kwa beki huyo sehemu za paja, hakutomfanya asimtumie kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambayo yataraji kuanza kutimua vumbo lake juma lijalo huku Man City wakitarajia kuanza na Blackburn Rovers.

Akizungumza na vyombo vya habari kupitia televisheni ya klabu ya Man City Hughes amesema anaamini Toure atapatiwa matibabu ya haraka na jopo la madakratri klabuni hapo hatua ambayo itamrejesha mapema kikosini.

Katika hatua nyingine meneja huyo amesema bado ana matumaini ya kumsajili beki wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Everton Joleon Lescott.

Hughes amesema bado wanaendelea na taratibu za kuushawishi uongozi wa klabu ya Everton ili uweze kukubalia kumuachia beki huyo.

No comments:

Post a Comment