Sunday, August 9, 2009

ULAJI WAMNYEMELEA TUNNER.


Meneja wa klabu ya Liverpool Rafael Benitez ameweka wazi mapenzi yake ya kutaka kumsajili beki wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Hull City Michael Turner.

Benitez ameyaanika wazi mapenzi hake kwa beki huyo, kufuatia kuumia kwa beki wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Jamie Carragher katika mchezo wa kirafiki uliounguruma jana dhidi ya Atletico Madrid ambapo mchezo huo ulimalizika kwa majogoo wa jiji Liverpool kubamizwa mabao mawili kwa moja.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo uliounguruma kwenye uwanja wa Anfiled, Benitez amesema tayari ameshaanza kufanya mazungumza na uongozi wa klabu ya Hull City ili kuweza kumsajili Michael Turner.

Meneja huyo toka nchini Hispania amesema mara kadhaaa amekuwa akizungumza na meneja mwenzake wa klabu ya Hull City Phil Brown, ambapo amebaini kwamba ana imani watafikia muafaka.

Hata hivyo tayari Beniteza ameshatangaza ofa ya paund million 6 kwa lengo la kutaka kumsajili Tunner, lakini uongozi wa klabu ya Hull City umetangaza bayana kutaka kiasi cha paund milion 12 kama ada ya uhamisho wa beki huyo.

Mbali na kumuwania beki huyo, meneja huyo ameripotiwa kuendelea na taratibu za kutaka kumsajili beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa na klabu ya Portsmouth Sylvain Distin.

Benitez yupo mawindoni kuwasaka mabeki kufuatia kuondoka kwa Sami Hyypia pamoja na Alvaro Arbeloa huku Daniel Agger na Martin Skrtel wakiuguza majeraha na huenda wakaikosa michezo ya mwanzo ya ligi kuu.

No comments:

Post a Comment