KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, October 28, 2010

Bongani Khumalo AJINASIBU.


Beki aliesajiliwa na klabu ya Tottenham Hotspurs Bongani Khumalo ameahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha anacheza katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza, ligi ya ambingwa barani ulaya pamoja na michuano ya kombe la FA.

Bongani Khumalo toka nchini Afrika kusini ambae ataianza safari ya kuelekea nchini Uiungereza mwezi Januari mwaka 2011 akitokea kwenye klabu yake ya Super Sports Utd kwa ada ya uhamisho wa paund million 1.5 amesema anaamini hilo linawezekana licha ya kutarajia upinzani mkali kutoka kwa wenyeji wake.

Amesema anatambua katika nafasi ya ulinzi ya Spurs wapo mabeki mahiri kama William Gallas, Ledley King, Sebastian Bassong pamoja na Michael Dawson lakini hana budi kukukabiliana nao na kujihakikishai nafasi katika kikosi cha kwanza.

Bongani Khumalo mwenye umri wa miaka 23, amesema umri wake bado mdogo hivyo suala hilo la kuwania nafasi katika kikosa cha kwanza linawezekana kufuatia kuwa na mustakabali mzuri katika mchezo wa soka.

No comments:

Post a Comment