KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, October 27, 2010

KIFO CHA PWEZA PAULO CHAZUA UTATA.


Siku moja baada ya kifo cha Pweza Paulo kilichotokea nchini ujerumani, taarifa za kushtukiza juu ya kifo cha kiumbe huyo zimeibuka huku ikidai kwamba taarifa zilizotolewa hazikua sahihi.

Taarifa hizo za kupinga kifo cha Pweza Paulo zimetolewa na muongoza filamu wa kimataifa toka nchini China Jiang Xiao ambapo amesema kumekua na udanganyifu juu ya ukweli wa kifo cha kiumbe huyo aliekua akifugwa huko nchini Ujeumani.

Jiang Xiao amesema wajerumani aliokua wakimfuga Pweza Paulo wamekua wakiufanya umma wa walimwengu ni wa kipuuzi juu ya taarifa za kifo ambapo yeye binafsi amedai Pweza huyo alikufa siku mbili kabla ya kuchezwa kwa mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la dunia yaani July 9.

Hata hivyo mwana mama huyo toka nchini China amedai kwa sasa bado anaendelea na uchunguzi wa kifo cha kiumbe huyo ambao unaendelea kumthibitishia kwa asilimia 60 hadi 70 kwamba kifo chake kilitokea July 9.

Mwana mama huyo amedai kwamba baada ya kukamilisha uchunguzi wake anatarajia kutoa filamu ambayo itaonyesha ukweli wa maisha ya Pweza huyo, na nini kilichopelekea kifo chake ambacho anaamini hakikuwa cha kawaida zaidi ya mtu kumdhuru.

No comments:

Post a Comment