KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, October 27, 2010

Michael Owen KUENDELEA KUWA NJE.


Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Man Utd Michael Owen amewapa matumaini mashabiki wake kwa kuwaeleza huenda akarejea tena uwanjani baada ya majuma kadhaa kufuati maumivu ya nyonga yanayomkabili kwa sasa.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool, Real Madrid pamoja na Newcastel Utd amesema anatambua mashabiki wake kwa kipindi kirefu wamekua wana hamu ya kumuona lakini ukweli ni kwamba bado anasumbuliwa na maumivu ya nyonga.

Amesema toka alipopata maumivu hayo katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Sunderland uliochezwa Oktoba 2 mwaka huu, amekua akiendelea vyema huku akipatiwa matibabu.

Hata hivyo juma lililopita meneja wa klabu ya Man Utd Sir Alex Ferguson alitangaza kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alitarajiwa kuanza mazoezi na alitarajia kumpa nafasi katika mchezo wa jana wa kuwania ubingwa wa kombe la ligi dhidi ya ya Wolves.

Akizungumzia hatua ya maamuzi yaliyofanywa na Wayne Rooney ya kuendelea kubaki klabuni hapo baada ya kukubalia kusaini mkataba wa miaka mitano, Michael Owen amesema amefurahishwa na hatua hiyo ambayo itaendelea kumfanya acheze na mchezaji wenye kiwango cha hali ya juu.

Licha ya kukiri kuwa na furaha ya mshambuliaji huyo kuendelea kubaki, pia Owen amesema ana hakika Rooney nae amefurahishwa na kitendo hicho cha kufanya maamuzi ya kuendelea kuitumikia klabu ya Man Utd.

Pia amezungumzia utaratibu wa kiungwana uliotumiwa na mshambuliaji huyo wa kuomba radhi huku akikiri kufanya makosa ambayo yalimkarahisha yoyote yule duniani anaeipenda Man Utd.

No comments:

Post a Comment