Pweza Paulo aliejizolea umaarufu wa kutabiri michezo ya fainali za kombe la dunia zilizochezwa nchini Afrika kusini mwaka huu, ameripotiwa kufariki dunia huko nchini ujerumani.
Taarifa kutoka kwa kuongozi wa mahala alipokua akihifadhiwa pewaza huyo Stefan Porwoll zimeeleza kuwa Pweza Paulo alifikwa na umauti usiku wa kuamkia hii leo na kifo chake ni cha kawaida na wala hakudhuriwa na yoyote yule.
Stefan Porwoll amesema Pweza Paulo amefikwa na umauti ghukua kiwa na umri wa miaka miwili ambapo safari yake ya maisha ilianza mwezi januari mwaka 2008 huko Weymouth nchini Uingereza.
Kama itakumbukwa vyema Pweza Paulo alitabiri uzuri matokeo ya michezo ya hatua ya makundi ya nchi ya Ujerumani ambapo alitabiri ushindi kwa nchi katika mchezo dhidi ya Australia waliokubali kichapo cha mabao manne kwa moja, katabiri mchezo dhidi ya Serbia ambapo ujerumani walilabwa bao moja kwa sifuri kisha akatabiri mchezo wa mwsiho wa hatua ya makundi dhidi ya Ghana waliokubali kichapo cha bao moja kwa sifuri.
Pweza Paulo aliingia katika matatizo mkubwa ya kuchukuwa na mashabiki wa soka nchini Uingereza baada ya kuitabiria timu ya taifa ya nchi hiyo kufungwa na timu ya taifa ya Ujerumani katika mchezo wa hatua ya 16, hatua mbayo ilifanikiwa baada ya timu ya taifa ya Uingereza kufungwa mabao manne kwa moja.
Pweza Paulo pia akaendelea kuitabiria vyema Ujerumani katika mchezo wa hatua ya robo fainali kwa kuitabiria kuifunga Argentina, na alifanikiwa katika utabiri huo lakini aliingia katika chuki kubwa dhidi ya mashabiki wa soka wa nchini Ujerumani kwa kuitabiria ushindi Hispania katika mchezo wa hatua ya nusu fainali na hilo lilitimia kwa Hispania kushinda bao moja kwa sifuri.
Katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia Pweza Paulo aliitabiria ushindi Hispania kutwaa ubingwa wa michuano hiyo na alifanikiwa baada ya Adres Iniesta kuifungia nchi yake bao pekee na la ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi.
No comments:
Post a Comment