KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, October 26, 2010

David Beckham AENDELEA KUIOTA UINGEREZA.


Kiungo wa klabu ya LA Galax ya nchini Marekani David Beckham bado ana ndoto za kuichezea timu ya taifa ya Uingereza licha ya kocha mkuu wa timu hiyo Fabio Capello kuonyesha nia ya kumtema katika kikosi chake.

David Beckham ameonyesha kuwa na ndoto hizo kufuatia mazungumzo aliyoyatoa mbele ya vyombo vya habari kwa kusema bado ana matumaini ya kumshawishi Capello ili aweze kumuita katika kikosi chake kinachoendelea na mikakati ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Ulaya za mwaka 2012.

Amesema kwa sasa anaendelea kujituma vilivyo akiwa na kikosi cha klabu yake ya LA Galax na mwishoni mwa juma aliisaidia klabu hiyo kufanya vizuri katika ligi ya nchini Marekani hivyo anaamini kocha huyo toka nchini italuia na mfuatilia na atamuita kwenye kikosi chake.

Hata hivyo Beckham ameongeza kuwa suala la umri kwake si kikomo cha kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa lake kwani bado anajiona ana nguvu za kuendelea kucheza soka la kisasa kama ilivyo kwa wachezaji mwingine.

Beckham mwenye umri wa miaka 35 tayari ameshaichezea timu ya taifa ya Uingereza michezo 115 na kwa mara ya mwisho ameitumikia timu hiyo mwezi Oktoba mwaka 2009 katika mchezodhidi ya timu ya taifa ya Belarus iliyokubalia kisago cha mabao matatu kwa mtungi.

No comments:

Post a Comment