Ushindi wa kwanza uliopatikana baada ya michezo saba kupita na kumuachia majonzi makubwa, hatimae meneja wa klabu ya Liverpool Roy Hodgson amenyanyua sauti na kuzungumza kwa furaha kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja uliopatikana jana huko Anfiled.
Hodgson ambae siku zake zilikua zinahesabika huko Anfield amesema kwa ushindi huo wa jana ana imini kikosi chake kimerejea katika hali ya kawaida na sasa kilichosalia ni kurejesha heshima ya Liverpool iliyokua imeyumba kutokana na vichapo na matokeo ya sare yaliyokua yamewaandama.
Amesema juhudi na kujituma kwa wachezaji wake hapo jana ndio ilikua silaha tosha ya kuwaangamiza wapinzani wao Blackburn Rovers ambao hata hivyo amewasifia walicheza kandanda safi wakati wote.
Katika hatua nyingine mzee huo wa kiingereza amempa tano mshambuliaji wake wa kimataifa toka nchini Hispania Ferdinando Torres kwa kuonyesha umahiri wa kufunga bao lake la kwanza toka msimu huu ulipoanza kati kati ya mwezi August.
Bao la kwanza la Liverpool katika mchezo huo lilipachikwa wavuni na beki wa kimataifa toka nchini Ugiriki Sotirios Kaigiakos katika dakika ya 48 na bao la pili likafungwa na Ferdinando Torres katika dakika ya 53 huku bao la kufutia mchozi la Blackburn Rovers likifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool El-Hadji Diouf katika dakika ya 51.
No comments:
Post a Comment