KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, October 25, 2010

PULIS AMUWAKIA MUAMUZI.


Meneja wa klabu ya Stoke City Tony Pulis amesema hakufurahishwa hata kidogo na maamuzi yaliyotolewa Andre Marriner aliechezesha pambano la jana ambalo lilishuhudia vijana wake wakizamishwa kwa idadi ya mabao mawili kwa moja na mashetani wekundu Man utd.

Tony Pulis amesema kitendo kilichimuudhi hadi kufikia hatua ya kulizungumza suala hili katika vyombo vya habari ni hatua ya muamuzi huyo kushindwa kumuadhibu beki wa pembani wa klabu ya Man utd Gary Neville baada ya vibaya mchezaji wake Matthew Etherington kwa makusudi.

Amesema beki huyo ambae jana alikua akiitumikia Man utd katika mchezo wa 600 alipaswa kuadhibiwa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu lakini Andre Marriner alimuacha huku akimuonya kwa kadi ya njano.

Hata hivyo meneja huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza amebinisha kwamba endapo vitendo hivyo wangekua wamevifanya wachezaji wake tena wakiwa ugenini huko Old Trafford adhabu zingetolewa kwa urahisi.

Nae beki wa klabu ya Man Utd Gary Neville amezungumzia hali hiyo kwa kusema kwamba hakufanya baya lolote la kupewa kadi nyekundu katika mchezo huo huku akikiri kadi ya njano aliyopewa na muamuzi Andre Marriner ilikua sahihi.

No comments:

Post a Comment