Wachezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Samson Siasia pamoja na Stephen Keshi wanapewa nafasi kubwa ya kuifundisha timu hiyo mara baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Iran utakaochezwa mwezi Novemba.
Magwiji hao wa soka nchini humo wanatarajiwa kufanyiwa usahili Novemba 4 na uongozi wa shirikisho la soka nchini Nigeria na mmoja kati yao atatangazwa kuchukua kazi ya kukinoa kikosi cha nchi hiyo.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini Nigeria Deji Tinubu amesema maamuzi ya kuwafikiria magwiji hao wawili kukinoa kikosi cha nchi hiyo yamefikiwa baada ya kuona upo umuhimu wa kikosi chao kunolewa na mzawa.
Hata hivyo Deji Tinubu amesema wakati wakiendelea na mchakato wa kutaka kuwafanyia usahili akina Samson Siasia pamoja na Stephen Keshi bado Austin Eguavoen ataendelea kushikilia kwa muda nafasi ya kukinoa kikosi cha Nigeria ambacho tayari ameshakitaja kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Iran.
Timu ya taifa ya Nigeria inarejeshwa mikononi mwa wazawa baada ya kunolewa na kocha wa kimataifa toka nchini Sweden Lagerback kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka huu ambapo haikufanya vyema baada ya kutolewa katika hatua ya makundi.
Samson Siasia pamoja na Stephen Keshi tayari wameshaitumikia timu ya taifa ya Nigeria kama wachezaji na walikua miongoni mwa wachezaji walioipa mafanikio nchi hiyo ya kutwaa ubingwa wa fainali za bara la Afrika mwaka 1994 pamoja na kuifikisha nchi hiyo kwenye hatua ya 16 bora katika fainali za kombe la dunia za mwaka huo zilizochezwa nchini Marekani.

No comments:
Post a Comment