KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, October 28, 2010

Nicklas Bendtner AJITETEA.


Mshambulaliji wa klabu ya Arsenal Nicklas Bendtner amesema hakuafanya kusudi kumzuai beki wa klabu ya Newcastle Utd alipokua akivunja hatua ya ya kuotea wakati Theo Walcot alipokua akienda kumsali kipa wa klabu ya the Magpies kwa kumbamiza bao la pili kwenye mchezo wa jana wa kombe la ligi.

Nicklas Bendtner amesema kama itatazamwa vyema picha ya mchezo huo wa jana itabainika kwamba alipokua akivunja hatua ya kuiotea kwa bahati mbaya aligongana na beki wa Newcastle ambae alikua akijaribu kumfukuza Theo Walcot ambae ytayari akuwa ameshamfikia kipa wa klabu ya Newcastle.

Mshambuliaji huyo ambae apia amecheza mchezo wa pili toka aliporejea uwanjani akitokea katika benchi la Majeruhi pia ameelezea furaha yake ya kurejea uwanjani nakufunga katika michezo yote.

Nae meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kwa kiasi kikubwa wachezaji wake alionyesha uwezo wa kuwakabili wapinzani wao aktika mchezo huo wa jana usiku licha ya Newcastle kuzuia kwa asilimia kubwa katika kipindi cha kwanza ambacho kilimaliza kwa Arsenal kuongoza bao moja kwa sifuri.

Arsene wenger pia ameonyesha kukunwa na umahiri wa mshambuliaji wake wa pembeni Theo Walcot ambapoa memuelezea kuwa ni mchezajia mbae anakua vyema na kila kukicha amekua akionyesha radha tofauti ya mchezo.

No comments:

Post a Comment