Kiungo wa klabu ya Metalist Kharkiv ya nchini Ukraine Sani Kaita amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria ambacho Novemba 17 kitakabiliwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Iran.
Kiungo huyo amejumuishwa katika kikosi cha Nigeria, ikiwa ni mara yeka ya kwanza toka alipoonyweshwa kadi nyekundu kwenye fainali za kombe la dunia katika mchezo dhidi ya Ugiriki.
Msemaji wa shirikisho la soka nchini Nigeria Robinson Okosun amesema kuitwa kwa Kaita kunamaanisha mchezaji huyo hajatengwa kutokana na makosa aliyoyafanya kwenye fainali za kombe la dunia hivyo wanaendelea kumthamini na kuuthamini mchango wake katika taifa la Nigeria.
Msemaji huyo pia amebainisha kwamba kikosi hicho cha wachezaji 20 kimeitwa na kocha Austin Eguavoen alierejeshewa mikoba yake mara baada ya kuondoka kwa Lars Lagerbäck toka nchini Sweden.
Kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kilichoitwa kwa ajili ya kuivaa timu ya taifa ya Iran huko mjin Tehran Nevemba 17 kinaundwa na wachezaji 13 kutoka kwenye klabu za ulaya na wachezaji saba wanacheza katika ligi ya nyumbani.
Makipa: Dele Aiyenugba (Bnei-Yehuda, Israel), na Bassey Akpan (Heartland)
Mabeki: Emmanuel Anyanwu, Valentine Nwabili (Enyimba), Dele Adeleye (Metalurh Donetsk, Ukraine), Chibuzor Okonkwo (Heartland), Taye Taiwo (Olympique Marseille, France), Abdulwasiu Showemimo (Kano Pillars), Michael Odibe (Siena, Italy).
Viungo: Kalu Uche (Almeria, Spain), Eneji Otekpa (Enyimba), Fengor Ogude (Valerenga, Norway), Sani Kaita (Metallist Donetsk, Ukraine), Ayo Saka (Ocean Boys).
Washambuliaji: Ahmed Musa (VVV Venlo, Holland), John Owoeri (Heartland), Obafemi Martins (Rubin Kazan, Russia), Osaze Odemwingie (West Bromwich Albion, England), Edward Ofere (Lecce, Italy), Obinna Nsofor (West Ham, England).
No comments:
Post a Comment