Uongozi wa chama cha soka nchini Zimbabwe umethibitisha taarifa za kufukuzwa kazi kwa mtendaji mkuu wa chama hicho Henrietta Rushwaya.
Taarifa ya uongozi wa chama hicho imeeleza kuwa Rushwaya ametimuliwa kazi kufuatia kuwa na utendaji mbovui wa kazi zake hatua mbayo imekiyumbisha chama hicho kwa kipindi kirefu.
Kosa kubwa lilimuweka kitimoto Henrietta Rushwaya na kufikia hatua ya kutimuliwa kazi ni upangaji wa matokeo ya timu ya taifa ya Zimbabwe ambayo ilifanya ziara barani Asia mwezi Disemba mwaka 2009 ambapo uchunguzi umebaini ni kweli hatua hiyo ilikuwepo huku mkono wa kiongozi ukihusika.
Uchanguzi uliofanywa na kamati maalum iliyoundwa na uongozi wa chama cha soka nchini Zimbabwe umekamilisha uchunguzi wake na kubaini kosa hilo kufuatia viapo walivyoapa baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ambao wamekiri kulipwa kiasi cha dola za kimarekani 500 hadi 1,500 ili waweze kujifungisha makusudi katika mchezo dhidi ya Thailand pamoja na Malaysia.
Mbali na kufukuzwa kazi ndani ya chama cha soka nchini Zimbabwe, kiongozi huyo pia amefungiwa kutojishughulisha na masuala ya soka katika nchi za ukanda wa Afrika kusini.
No comments:
Post a Comment