Jeshi la Ashburton Grove Arsenal lenyewe litafunga safari kuelekea huko DW Stadium kupambana vilivyo na wenyeji wao Wigan Athletics.
Arsenal wanakwenda ugenini hii leo huku akiwa wanachagizwa na ushindi wa mabao matatu kwa moja walioupata mbele ya Chelsea siku mwanzoni mwa juma hili ambapo inaamikika hatua hiyo itawaongezea chachu ya kuhakikisha wanazipata poit tatu muhimu za mchezo huo.
Hata hivyo Arsenal wanamkosa nahodha na kiungo wao wa kimataifa toka nchini Hispania Cesc Fabregas ambae anatumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi tano za njano ambazo zilitimia katika mchezo dhidi ya Chelsea baada ya kumfanyia madhambi kiungo wa klabu hiyo ya Stamford Bridge.
Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger tayari ameshaeleza wazi kwamba usiku huu ana matumaini makubwa ya kumtumia kiungo wa kimataifa toka nchini Urusi Andrey Arshavin, mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Morocco Marouane Chamakh pamoja na beki wa kimataifa toka nchini ufaransa Sebastien Squillaci ambao walishindwa kuwaanzisha kwenye kiksoi cha kwanza mwanzoni mwa juma hili.
Kwa upande wa Wigan wao wanaingia katika uwanja wa nyumbani hii leo huku wakiwa na kumbu kumbu ya ushindi wa mabao mawili kwa moja walioupata mbele ya Wolveshampton Wanderers mwishoni mwa juma lililopita.
Meneja wa klabu ya Wigan Roberto Martinez tayari ameshavieleza vyombo vya habari kwamba mchezo wa hii leo utakua mgumu sana, hasa ikizingatia anakabiliwa na wachezaji majeruhi pamoja na wale wanaotumikia adhabu.
Amesema anatambau wanakwenda kupambana na kikosi cha Arsenal ambacho kina morari ya kuendeleza mazuri yaliyopatikana katika mchezo uliopita dhidi ya Chelsea, hivyo wamejiandaa kwa hilo na ana imani mtihani huo wataushinda.
Katika mchezo huo wachezaji wa kimataifa toka nchini Honduras Hendry Thomas pamoja na Maynor Figueroa wote wanatarajia kujumuishwa kikosini baada ya kutumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi tano za njano huku Emmerson Boyce pamoja na Franco Di Santo wakiwa bado ni majeruhi.
No comments:
Post a Comment