Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amelazimika kumbwatukia wazi wazi beki wake wa kimataifa toka nchini Ufaransa Younes Kaboul baada ya kuchukizwa na kitendo cha kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi uliochezwa jana dhidi ya Newcastle Utd.
Harry Redknapp alilazimika kufanya hivyo huku akidai kwamba Younes Kaboul hakustahili kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo huo hasa ukizingatia kosa lililopelekea kukutwa na adhabu hiyo.
Amesema kulikua hakuna haja ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kuendelea kujibishana na kiungo wa klabu ya Newcastle Utd Cheik Tiote baada ya kumchezea ovyo, lakini Kaboul aliendelea kuomnyesha utovu wa nidhamu ambao ulisababishwa aadhibiwe na muamuzi.
Mzee huyo wa kiingereza emedai kwamba mara kadhaa mchezaji anapokua uwanjani anatakiwa kuwa na nidhamu ya kutosha kwa maslahi ya klabu kwa ujumla na anatakiwa kufahamu endapo atakwenda kinyume na utaratibu huo kuna uwezekano mkubwa wa kuigharimu timu.
Wakati Harry Redknapp, akimbwatukia Younes Kaboul huku kikosi chake kikiwa kimefaidika na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri katika mchezo wa jana, meneja wa klabu ya Newcastle utd Alan Pardew, ameonyesha kuridhishwa na kiwango kizuri kilichoonyesha na kikosi chake ambacho kimepoteza mchezo wa pili mfululizo.
Amesema kwa ujumla kikosi chake kilicheza vizuri na kilikua na kila sababu za kuibamiza Spurs lakini mapungufu yaliyojitokeza katika safu ya ushambuliaji yaliwagharimu kwa kiasi kikubwa hasa zilipojitokeza nafasi za kumalizia mipira kuingai nyavuni.
Alan Pardew aliekabidhiwa kikosi cha The Magpies mara baada ya kutimuliwa kazi kwa Chris Hughton mwanzoni mwa mwezi huu ameendelea kueleza kwamba kwa 100% ya mabao ya wapinzani wao yaliyopatikana katika mchezo huo wa jana yalitokana na makosa yaliyofanywa na safu yake ya ushambuliaji ambayo haikuwa na umakini wa kutosha.
No comments:
Post a Comment