KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 25, 2010

Ashley Cole AICHIMBA MKWARA ARSENAL.


Aliekua beki wa pembeni wa klabu ya Arsenal Ashley Cole amechimba mkwara kwa wachezaji wa klabu hiyo ya kaskazini mwa jiji la London kwa kuwaeleza wasitegemee mteremko katika mchezo wao wa jumatatu ambao utapigwa huko Emirates.

Ashley Cole ambae aliondoka Arsenal mwaka 2006 na kujiunga na Chelsea amepiga mkwara huo huku akieleza wazi kwamba kikosi chao kwa sasa kipo kamili hivyo ana imani mtitiriko wa ushindi unaanza siku ya jumatatu mbele ya The Gunners.

Amesema wanakwenda katika mchezo huo huku wakiwa na kumbu kumbu mbaya ya kutokufanya vyema kwenye michezo yao ya mwezi uliopita hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanarejesha matumaini kwa mashabiki wao.

Sababu kubwa iliyotolewa na beki huyo mwenye umri wa miaka 30, ya kujiamini wataanza kupata ushindi katika mchezo huo wa siku ya jumatatu ni kurejea kwa asilimia kubwa ya wachezaji wao waliokua majeruhi, hatua ambayo ameitaja kuwa chanzo cha kutokufanya vyema kwenye michezo yao ya mwezi uliopita.

Nae meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti amesema amekiandaa kikosi chake kwa minajili ya kupata point tatu muhimu kuanzia mchezo dhidi ya Arsenal, Bolton kisha Aston Villa.

Kwa upande wake meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema inawalazimu kushinda mchezo huo wa jumatatu kwa ajili ya kurekebisha makosa yaliyojitokea katika mchezo wao dhidi ya Man Utd ambao ulishuhudia wakipoteza point tatu kwa kufungwa bao moja kwa sifuri.

Amesema ana imani suala hilo linawezekana kufuatia uwezo wao wa kisoka kupanda wanapocheza nyumbani mbali na siku kadhaa ziliopita, lakini mzee huyo akaonyesha kuamini kwamba matumaini ya kuendelea kuwepo katika mbio za ubingwa bado yapo mikononi mwao hasa katika mchezo wa Chelsea pamoja na ule wa Man utd ambao pia utapigwa kaskazini mwa jiji la London.

No comments:

Post a Comment