Meneja wa klabu ya Everton David Moyes ameelezea matumaini yake ya kumbakisha kiungo wa kimataifa toka nchini Afrika kusini Steven Jerome Pienaar ambae anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na Tottenham Hotspurs.
David Moyes ameelezea matumaini hayo huku akitambua fika mkataba wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.
Amesema bado anamuhitaji Steven Jerome Pienaar kwenye kikosi chake hivyo anaendelea kumshawishi kuhakikisha dhamira yake inatimia na ana imani suala hilo litafanikiwa na kumsainisha mkataba mpya.
Amesema mara kadhaa mchezaji anaposalia na mkataba wa mwaka mmoja masuala mengi hutazamwa na meneja wa klabu husika na ikibainika mchezaji huyo hana sifa za kutosha kuachiwa aondoke lakini kwa Steven Jerome Pienaar anaona bado kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuwa nae.
No comments:
Post a Comment