KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 16, 2010

Bertrand Marchand AONYESHA MASIKITIKO YAKE HADHARANI.


Kocha wa kimataifa toka nchini Ufaransa Bertrand Marchand amesema amesikitishwa na hatua na kitendo cha shirikisho la soka nchini Tunisia cha kusikitisha mkataba wake wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo The Carthage Eagles.

Akielezea masikitiko yake alipozungumza na vyombo vya habari vya huko nchini Tunisia, kocha huyo mwenye umri wa miaka 57 amesema kubwa lililomsikitisha ni kuharibiwa mipango ambayo tayari alikua ameshaiwasilisha kwa viongozi wa shirikisho la soka nchini humo.

Amesema miongoni mwa mipango aliyoiwasilisha katika ofisi za shirikisho la soka nchini Tunisia ni pamoja na mipango ya muda mfupi na ile ya muda mrefu ambayo aliamini ingeiwezesha nchi hiyo kufikia malengo iliyojiwekea kuanzia msimu huu wa kuelekea kwenye fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2012.

Amesema mipango ya muda mfupi ilikua ni kukitumia kikosi kilichopo kwenye michezo ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za mwaka 2012 za barani Afrika na mipango ya muda mrefu ni kutumia baadhi ya wachezaji wa kikosi cha vijana kwenye fainali hizo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuelekea nchini Brazil kwenye fainali za kombe la dunia.

Kibarua cha Bertrand Marchand kiliota nyasi jana siku ya jumatano, baada ya kamati kuu ya shirikisho la soka nchini Tunisia kukutana na kuafikiana kwa pamoja kutimuliwa kazi kwa mfaransa huyo ambae amepata matokeo mabovu kwenye michezo miwiwili ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika ambapo katika mchezo wa kwanza The Carthage Eagles walibamizwa na Botwana kabla ya kutoka sare nyumbani na timu ya taifa ya Malawi.

Bertrand Marchand aliingia mkataba wa miaka miwiwli wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tunisia mwezi June mwaka huu akitokea nchini Qatar alipokua akiifundisha klabu ya Alkhor.

No comments:

Post a Comment