Katibu mkuu wa shirikisho la soka duniani kote FIFA Jerome Valcke amesema tarehe rasmi ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022, inatarajiwa kujulikana juma lijalo baada ya viongozi wa shirikisho hilo kukuna na viongozi wa shirikisho la soka barani Asia AFC.
Valke ametoa uthibitisho huo alipozungumza na waandishi wa habari huko Abu Dhabi zinapofanyika fainali za klabu bingwa dunini ambapo amesema viongozi wa pande hizo mbili watatiliana saini katika mikataba maalum ambayo itaainisha wazi tarehe rasmi ya kufanyika kwa fainali za kombe la dunia.
Amesema tayari mjumbe wa kamati kuu ya FIFA Franz Beckenbauer, ameshauri fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 zitapendeza endapo zitachezwa mwanzoni mwa mwaka huo kufuatia hali ya hewa ya nchini Qatar kwa kipindi hicho itakuwa chini ya nyuji joto 40.
Ufafanuazi huo kutoka kwa katibu mkuu wa FIFA umetolewa kufuatia hofu iliyotanda kwa mashabiki wa soka duniani ambao wanahofia msimu wa joto endapo fainali za kombe la dunia zitapangwa kuchezwa mwezi june kama ilivyo kawaida.
Hofu ta msimu wa joto ilitanda baada ya mwenyekiti wa shirikisho la soka barani Asia Mohamed Bin Hammam kuonyesha wasi wasi wake juu ya msimu huo ambapo aliwashauri FIFA kuzisogeza nyuma fainali hizo ili ziweze kuchezwa mwei Januari ama mwezi Februari mwaka 2022 kipindi ambacho hupatikana hali ya hewa ya kuridhisha.
No comments:
Post a Comment