KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, December 27, 2010

Bongani Khumalo KUIANZA SAFARI YA ULAYA.


Safari ya beki wa kimataifa toka nchini Afrika kusini na klabu ya Super Sports Bongani Khumalo ya kuelekea nchini Uingereza kujiunga na klabu ya Tottenham Hotspurs ipo katika hatua za mwisho kufuatia beki huyo kuwa kwenye heka heka za kutafuta kibali cha kuinga kwenye nchi zilizo chini ya utawala wa Malkia Elizabeti.

Wakala wa beki huyo mwenye umri wa miaka 23 Glyn Binkin, amesema tayari wameshapeleka maombi ya kibali hicho na wana matumaini siku za hivi karibuni mambo yatakua mazuri hivyo mchezaji wake ataianza safari ya kuelekea nchini Uingereza tayari kwa kujiunga na klabu yake mpya.

Amesema wamekua na mawasiliano mazuri na uongozi wa Spurs na ama matumaini makubwa Khumalo atakapofika nchini Uingereza ataebndeleza yale yote mazuri aliyokua akiyafanya kwenye klabu yake ya Super Sports iliyokubali dili la kumuuza kwa ada ya uhamisho wa paund million 1.5.

Bongani Khumalo anakwenda kujiunga na Spurs kupitia usajiliw a dirisha dogo ambao utaanza kuchukua mkondo wake mwanzoni mwa mwezi ujao katika ukanda wa barani Ulaya.

Siri na mafanikio makubwa ya beki huyo kusajiliwa na Spurs, ni baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na Bafana Bafana wakati wa fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Afrika kusini na kushuhudia timu ya taifa ya Hispania ikiibuka bingwa.

No comments:

Post a Comment