Meneja wa klabu ya Fulham Mark Hughes ameonyesha kuridhia mamalamiko yanayotolewa na mashabiki wa klabu hiyo kufuatia kupoteza mchezo wa jana dhidi ya West Ham Utd ambao waliondoka Croven Cottege na ushindi wa mabao matatu kwa moja.
Mark Hughes ameonyesha kuridhishwa huko baada ya kueleza kwamba mashabiki hao wana haki na kuonyesha kuchukizwa na matokeo mabovu kutokana na kikosi cha timu yao kushindwa kufanya vyema katika uwanja wa nyumbani ambao ulikua na kila sababu za kuwabeba na kufikia malengo ya kubaki na point tatu muhimu.
Amesema hafahamu nini sababu ya kupoteza mchezo jana ili hali tayari walikua wameshaonyesha uwezo mkubwa wa kuwamiliki wapinzani wao katika dakika za mwanzo halia mbayo iliwasaidia kupata bao la kuongoza katika dakika ya 11 kupitia Aaron Hughes lakini cha kushangaza hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika walijikuta wamechapwa mabao matatu kwa moja.
Hata hivyo Mark Hughes amewataka mashabiki wa The Cottegers kupunguza hasira, huku akiwaahidi kufanya jitihada za kukiwezesha kikosi chao kupata ushindi katika siku za usoni ambapo anaamini atakuwa na wachezaji wake wote muhimu.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 47 amebainisha kwamba kurejea kwa Bobby Zamora pamoja na Andy Johnson kutaongeza chachu ya kufanya jitihada za kusaka ushindi hivyo bado anaamini kikosi chake kina nafasi ya kutosha.
Katika hatua nyingine meneja huyo wa kimataifa toka nchini Wales amekanusha taarifa za yeye kuwa mbioni kutimuwa klabuni hapo kufuatia kushindwa kutimiza malengo aliyowekewa na mmiliki wa klabu hiyo Mohameed Al-Fayed.
No comments:
Post a Comment